Na Joseph Lieme
Mauzo ya Hisa (Turnover/ Liquidity)
Thamani ya mauzo ya hisa yameongezeka kutoka Shilingi Billioni 5.4 ya wiki iliyoishia 15 Septemba 2017 hadi Shilingi Bilioni 53.5 kwa wiki iloyoishia 22 Septemba 2017,
Vile vile idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imeongezeka kutoka hisa Milioni 2 ya wiki iliyoishia 15 Septemba 2017 hadi hisa milioni 4 ya wiki iliyoishia 22 Septemba 2017.
Kampuni zilizoongoza katika mauzo ya hisa ni kama ifuatavyo:
TBL …………………………………………..……99%
VODA….…..…….………………..……………….…0. 22%
CRDB …………..…….....……….……....…………. 0.09%
Ukubwa Mtaji (Market Capitalization)
Ukubwa wa mtaji wa kampuni zilizoorodheshwa katika soko umeongezeka kwa Shilingi Bilioni 293 kutoka Shilingi Trilioni 20.2 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 20.5 wiki iliyoishia tarehe 22 Septemba 2017. Ongezeko hili limetokana na kupanda kwa bei za hisa za Kenya Airways (20%), USL (12.5%) na KCB (9%).
Ukubwa wa mtaji wa kampuni za ndani umeongezeka kwa Shilingi Milioni 27 hadi kafika Shilingi Trilioni 9.67 wiki hii. Hii ni kutokana na kupanda kwa bei ya hisa za TBL (0.75%).
Kampuni
|
22 September 2017 (Shilingi)
|
15 September 2017 (Shilingi)
|
Badiliko (%)
| ||||
CRDB
|
0.00%
| ||||||
DCB
|
0.00%
| ||||||
DSE PLC
|
1,300
|
-5.80%
| |||||
MBP
|
0.00%
| ||||||
MCB
|
0.00%
| ||||||
MKCB
|
0.00%
| ||||||
MUCOBA
|
0.00%
| ||||||
NMB
|
2,750
|
0.00%
| |||||
PAL
|
0.00%
| ||||||
SWALA
|
0.00%
| ||||||
SWIS
|
3,820
|
0.00%
| |||||
TBL
|
13,400
|
0.75%
| |||||
TCC
|
13,100
|
0.00%
| |||||
TCCL
|
1,360
|
0.00%
| |||||
TOL
|
0.00%
| ||||||
TPCC
|
1,780
|
0.00%
| |||||
TTP
|
650
|
0.00%
| |||||
VODA
|
0.00%
| ||||||
YETU
|
0.00%
| ||||||
Kampuni zilirodhodheshwa kutokea Masoko mengine
| |||||||
ACA
|
5,480
|
0.37%
| |||||
EABL
|
5,370
|
0.37%
| |||||
JHL
|
10,630
|
2.31%
| |||||
KA
|
20.00%
| ||||||
KCB
|
8.89%
| ||||||
NMG
|
2,180
|
-10.29%
| |||||
USL
|
12.50%
| ||||||
Mtaji Jumla Makampuni yote (Bilioni)
|
20,470
|
1.45%
| |||||
Mtaji Jumla Makampuni ya Ndani (Bilioni)
|
9,672
|
0.29%
| |||||
Kiashiria cha DSEI (pointi)
|
2,128
|
1.43%
| |||||
Kiashiria cha TSI (pointi)
|
3,715
|
0.30%
|
Viashiria (Indices)
Kiashiria cha kampuni zote zilizoorodheshwa katika soko yaani DSEI kimepanda kwa pointi 30 kutoka pointi 2,098 hadi pointi 2,128 kutokana na kupanda kwa bei za hisa za kampuni Kenya Airways, Uchumi Supermarket Ltd na Kenya Commercial Bank
Hata hivyo kishiria cha kampuni za ndani yaani TSI kimepanda kwa pointi 11 kutoka pointi 3,704 hadi pointi 3,715
Kiashiria cha sekta ya viwanda (IA) kimepanda kwa pointi 26 kutoka pointi 5052 hadi pointi 5078
Kiashiria huduma za kibenki na kifedha (BI) wiki hii imepungua kwa pointi 2 kutoka pointi 2,520 hadi pointi 2,518
Kiashiria cha Sekta ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii imebaki kama awali kwenye wastani wa pointi 2,475
Hati Fungani (Bonds)
Mauzo ya hati fungani katika wiki iliyoishia tarehe 22 Septemba 2017 yalikuwa Shilingi Bilioni 36 kutoka Bilioni 22 wiki iliyopita ya 15 Septemba 2017.
Mauzo haya yalitokana na hatifungani kumi na nne (14) za serikali zenye jumla ya thamani ya Shilingi Bilioni 40 kwa jumla ya gharama ya Shilingi Bilioni 36.
0 maoni:
Chapisha Maoni