Taarifa imesema…>>>’Kumekuwa na habari mbalimbali kuhusu Clouds Media Group na viongozi mbalimbali akiwemo Askofu Josephat Gwajima na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda. Kiini cha habari zote hizo ni uwepo wa taarifa zinazomhusu mwanamke anayedai kuzaa na Askofu Gwajima‘
‘Ni kweli habari ya uwepo wa mama huyo ilitufikia kupitia kipindi chetu cha De Weekend Chat Show (SHILAWADU) lakini baada ya uchunguzi wa kina tuligundua kwamba habari haina mashiko, inakosa vigezo vya habari inayofaa kuonyeshwa na hivyo tulisimama katika kanuni za taaluma yetu na kuzuia kabisa kuonyeshwa kwa taarifa hiyo‘
‘Kizuizi hicho kilifuatiwa na matukio mbalimbali ikiwemo mijadala inayosambaa juu ya Mkuu wa mkoa Paul Makonda kuvamia ofisizetu. Jambo hilo limezua hofu na taharuki kubwa kwa wadau wote pamoja na kusababisha mashaka miongoni mwa wafanyakazi na viongozi wa Clouds Media Group‘
‘Pamoja na yote jambo hili lipo katika uchunguzi wa kina unaofanywa na sisi Clouds Media Group kwa kushirikiana na mamlaka zote husika, tunaomba wapenzi, wadau na Watanzania wote wawe na subira wakati tunajiandaa kutoa tamko rasmi kuhusu yaliyotokea‘
0 maoni:
Chapisha Maoni