Kabla ya kuchukua hatua zozote, sisi kama Serikali tunataka kusikia kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Tumeunda timu ya watu 5 kufanya kazi kwa saa 24 ili wapate maelezo ya Mkuu wa Mkoa. Baada ya hapo tutasema hatua tutakazochukua (kama Serikali) “
” I am very proud of you ( #CloudsMediaGroup ), jambo hili mmelipeleka in a very professional way.
Jambo lilitokea lilikuwa kubwa na la kutisha lakini mpaka J1 mlitulia kama hakuna kilichotokea. Hali ilikuwa mbaya nilishapata taarifa kutoka kwa Waandishi wa mikoani wakitaka kuandamana. Lakini ninyi mmelinda amani ya nchi yetu na mkalipeleka jambo kwa utaratibu mzuri “
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Makampuni ya IPP Regnald Mengi ambaye pia ni Mwenyekiti wa wamiliki wa vyombo vya habari (MOAT) ameeleza yafuatayo.
“Jambo lililofanyika ni la hatari sana. Na lazima tujiulize mtu huyu ( Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ) anapata wapi ujasiri huu?. Kama alikuja na bunduki hapa anaweza kwenda nazo popote na pengine kuna siku atazitumia.
Mimi nina imani kwamba tuna Rais anayetupenda sana, na tuna Waziri anayetupenda sana. Lakini mapenzi hayo lazima yaonyeshwe kwa vitendo.
” Sura moja ya muandishi wa habari ni kutokuwa muoga. Jambo hili lililotokea lisifanye tukawa waoga. Wanahabari sio waoga.”
“Jambo lililofanyika ni la hatari sana. Na lazima tujiulize mtu huyu ( Mkuu wa Mkoa wa DSM ) anapata wapi ujasiri huu?
Kama alikuja na bunduki hapa anaweza kwenda nazo popote na pengine kuna siku atazitumia.”
@josephkusaga ni Mtoto wangu ninayempenda sana. Kuna wakati nilitaka ‘kumuadopt’ lakini akasema sasa jina langu itakuwaje? . Hilo lilishindikana lakini ni mwanangu, ninampenda sana “
0 maoni:
Chapisha Maoni