Rais John Magufuli amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuendelea kuchapa kazi na kwamba yeye hafanyii kazi maneno ya kwenye mitandao kwasababu yeye ndiyo Rais wa nchi hii.
Rais Magufuli amesema kuna baadhi ya watu wanaingilia majukumu yake wakati yeye ndiyo mwenye uamuzi na kwamba hapangiwi kazi ya kufanya kwa sababu anajiamini.
Mkuu huyo wa nchi amewataka wakazi wa Dar es Salaam kuchapa kazi ili kujiletea maendeleo badala ya kupoteza muda kufuatilia udaku kwenye mitandao.
"Watu wa Dar es Salaam tumejielekeza sana kwenye udaku ambao hausaidii maendeleo. Udaku ambao haumalizi hata foleni ya Dar.
"Ningefurahi sana huko kwenye mitandao kama tungekuwa tunajadili jinsi ya kufanya mambo ya maendeleo.
"Mimi sionyeshwi njia ya kupita na mtu. Njia ya kupita tayari nilishaonyeshwa na ilani ya chama changu.
"Kuandikwa kwenye mitandao hata mimi ninaandikwa, kwa hiyo nijiuzulu? Kuandikwa kwangu mimi siyo tija bali kuchapa kazi.
"Kuna wengine mmefikia hata hatua ya kunipangia. Nasema mimi ukinipangia ndio umeharibu
"Vitu ambavyo havina msingi vinachukua muda wetu mwingi sana. Mara upost hiki, mara uweke kile.
"Watanzania mjue kampeni zimeshakwisha. Ulie, ugaregare lakini Rais ni mimi John Pombe Magufuli na kwangu ni kazi tu.
"Mimi ni rais ninayejiamini, sipangiwi mambo ya kufanya. Hata fomu ya kugombea nilikwenda kuichukua peke yangu, kwa hiyo Makonda wewe chapa kazi,"amesema Rais Magufuli.
0 maoni:
Chapisha Maoni