Makonda ameyasema hayo leo katika wiki ya maji na kuongeza kuwa kuna baadhi ya sehemu watu wamekuwa wakiharibu miundombinu ya maji bila kutoa taarifa kwa mamlaka husika jambo linalopelekea uhaba wa maji katika maeneo hayo.
Amesema kwa kwa sasa jiji la Dar es Salaam lina uhitaji wa lita milioni 510 kwa siku ambapo lita 390 tu ndizo zinazozalishwa kwa sasa hivyo serikali imejipanga kipitia miradi yake mbalimbali ukiwepo ule wa Ruvu juu na chini mpaka kufikia mwaka 2020 tatizo la maji katika mkoa liwe limepungua kwa aslimia95%.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu shirika la Maji safi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASCO) Kiula Kingu ameeleza kuwa wiki tatu zinazokuja watajitahidi kushughulikia tatizo la maji kwa maeneo yote yaliyokumbwa na hadha hiyo ya ukosefu wa maji.
Wiki ya maji duniani huazimishwa kila tarehe 16-22 mwezi MachI ya kila mwaka ambapo mwaka huu kauli mbiu yake ni “Majisafi na Majitaka- Punguza Uchafuzi yatumike kwa ufanisi”
0 maoni:
Chapisha Maoni