WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Ijumaa, 2 Desemba 2016

 00:11      No comments

HOTUBA YA MHE. ANGELLAH J. KAIRUKI (MB.), WAZIRI WA NCHI, OFISI YA

RAIS- MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA KATIKA

UFUNGUZI WA MDAHALO WA WADAU KUHUSU KUJENGA NA KUKUZA

MAADILI, HAKI ZA BINADAMU, UWAJIBIKAJI, UTAWALA BORA NA

MAPAMABANO DHIDI YA RUSHWA, KATIKA UKUMBI WA MAKUMBUSHO YA

TAIFA, DAR ES SALAAM, TAREHE 30 NOVEMBA 2016.

Imesomwa na Naibu Katibu Mkuu UTUMISHI, Bi Susan Mlawi..
 
Awali ya yote ninapenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa

fursa hii kushiriki nanyi katika ufunguzi wa mdahalo huu wa wadau

unaohusu masuala ya Maadili, Haki za Binadamu, Uwajibikaji, Utawala

Bora na Mapambano Dhidi ya Rushwa.

Binafsi nimefarijika sana kupewa fursa hii na waratibu wetu wa Kampeni

ya Kukuza na Kujenga Maadili, Haki za Binadamu, Uwajibikaji, Utawala

Bora na Mapambano Dhidi ya Rushwa.


Nimealikwa ili kufungua mdahalo ambao ni wapili kwa mwaka huu

kufanyika kitaifa, ulioandaliwa mahsusi kwa ajili ya Wadau wa Maadili.

Nitumie nafasi hii kukushukuru wewe binafsi Kaimu Mwenyekiti wa

Kamati ya Maadhimisho pamoja na Wakuu wote wa Taasisi zinazoratibu

Kampeni hii kwa heshima kubwa mliyonipa, kunialika kwa nafasi ya

Mgeni Rasmi.

Pia ninapenda kuwapongeza wadau wote ambao mmeona ni vyema na

busara kutenga muda wenu kwa ajili ya kushiriki katika mdahalo huu.

Ni wahakikishie kuwa uwepo wenu hapa ni muhimu sana sio tu katika

kufanikisha malengo ya mdahalo huu bali pia katika kujenga utamaduni

wa kuthamini tunu za taifa letu ambapo Maadili nimiongoni mwa tunu

hizo.


Kama nilivyo kwisha kusema huu ni mdahalo wapili ambao unafanyika

baada ya Mdahalo wa Kwanza wa Tarehe 22 Novemba 2016 ambao

ulihuisha wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari. Midahalo hii ni

muhimu sana na imekuja wakati muafaka kwa kuwa Taifa letu lipo katika

changamoto kubwa ya kuhakikisha linajenga, kukuza na kusimamia

maadili kwa jamii nzima.

Nimefurahi kusikia kuwa, Kampeni kuhusu kujenga na kukuza Maadili,

Haki za Binadamu, Uwajibikaji, Utawala Bora na Mapambano dhidi ya

Rushwa imeendelea kufanikiwa, na mdahalo huu ni sehemu ya kampeni

hiyo.


Maadili ni hatua muhimu sana ambayo humtambulisha mtu ndani ya

jamii yake na katika hali ya kawaida Maadili hujitokeza katika matendo

kwa vile ndicho kilelezo sahihi cha kupima Maadili ya jamii. Kauli mbiu

yetu ni, “Kujenga na Kukuza Maadili, Haki za Binadamu, Uwajibikaji,

Utawala Bora na Mapambano Dhidi ya Rushwa”. Lengo la kuwa na

kauli mbiu hii ni kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya tano

inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kupinga

vitendo vya Rushwa, Uzembe, Ufisadi na Matumizi Mabaya ya Fedha za

Umma na Ukiukwaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu.


Maadili ni suala linalopewa kipaumbele na Serikali ya Awamu ya Tano.

Mtakubaliana na mimi kuwa Mhe. Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli

katika mikutano yake yote amekuwa akiwasihi sio tu watumishi wa

umma bali pia wananchi kwa ujumla kurudia Maadili yetu.

Katika kipindi chake cha mwaka mmoja wa uongozi amekuwa akionesha

kwa vitendo jinsi gani anachukizwa na ukiukwaji wa maadili, haki za

binadamu, ufisadi hata kukemea wazi wazi rushwa na harufu za rushwa

katika Serikali yake mwenyewe.


Mimi nikiwa Waziri wa Nchi, mwenyedhamana ya kusimamia Maadili

katika Utumishi wa Umma, sitaacha kutoa kipaumbele katika

kushirikisha jamii nzima kwa ujumla kupambana na vitendo vya

ukiukwaji wa Maadili, Haki za Binadamu, Uwajibikaji, Utawala Bora na

Mapambano Dhidi ya Rushwa.


Pamoja na majukumu mengi niliyopewa kuyatekeleza kwa nafasi hii,

bado niseme kwamba kutokana na umuhimu wa Mdahalo huu kwa jamii

au taifa letu katika kutimiza dhana ya utawala bora ambapo uwazi na

uwajibikaji ni nguzo muhimu ya Utawala Bora, suala la ushiriki na

ushirikishwaji wa wadau mbalimbali wa masuala ya Maadili ni lakupewa

kipaumbele hivyo niwaombe ndugu zangu kila mmoja kwa nafasi yake,

tusirudi nyuma tufanye sehemu yetu.


Ili kufanya suala la maadili lisiwe la kipindi cha kampeni tu, sisi wadau

wa masuala haya tunatakiwa kuelewa kuwa suala la Kujenga, Kukuza



na Kusimamia Maadili siyo jukumu la Mheshimiwa Rais wetu Dkt; John

P. Magufuli peke yake, au Taasisi za usimamizi peke yao au Viongozi

wa Dini, wala siyo jukumu la vyama vya siasa au vyombo vya dola

nchini, bali ni jukumu la jamii nzima. Hivyo, nitoe rai kwa jamii nzima

kuwa sote tushirikiane kwa pamoja katika ngazi zote na hasa sisi

tuliohudhuria leo tuwe mabalozi wa kwanza kufikisha ujumbe vizuri kwa

jamii.



Nimearifiwa kuwa katika mdahalo huu kutakuwepo na uwasilishwaji wa

mada mbalimbali ambazo zimeandaliwa ili kutoa muelekeo wa mjadala

mpana wa masuala ya Maadili, Haki za Binadamu, Uwajibikaji, Utawala

Bora na Mapambano Dhidi ya Rushwa, ni matarajio yangu kuwa wote

tutapata fursa ya kutoa michango itakayosaidia kuondokana na

changamoto nyingi za kimaadili zinazotukabili hivi sasa.


Sio siri kuwa kadiri siku zinavyoenda suala la maadili ni changamoto sio

tu kwa Tanzania bali hata dunia kwa ujumla. Vitendo vya Rushwa,

Ufisadi na Ukiukwaji wa Haki za Binadamu vimeendelea kuwa ni tatizo

la dunia nzima. Kwa mfano tatizo la Mauaji ya Kutisha ya ndugu zetu

wenye ulemavu wa ngozi kwa kiasi kikubwa linachangiwa na ukiukwaji

wa maadili. Je vyombo vya dola peke yake vinaweza kumaliza matatizo

haya? Ni ukweli usiopingika kuwa peke yake matatizo haya hayawezi

kumalizika. Tunahitaji jamii nzima ipinge, ikemee na kutokomeza vitendo

vyote vya ufisadi, rushwa, ukiukwaji wa maadili na haki za binadamu ili

kuliletea taifa letu maendeleo endelevu. Hii haimaanishi kuwa Serikali ya

Awamu ya Tano haitatekeza majukumu yake ya msingi katika kuhikiza

uzingatiaji wa maadili, la hasha, tutaendelea kuchukua hatua mbalimbali

za kinidhamu na kisheria ili kupunguza kama sio kumaliza matatizo

haya.


Serikali katika kipindi hiki cha uwepo wa mmomonyoko wa maadili

unaotokana na utandawazi na mambo mengine, imeendelea kutoa

maelekezo mbalimbali yanayolenga katika kurejesha nidhamu na

maadili kwa watumishi wa umma na jamii kwa ujumla kwa sababu

watumishi wa umma hawawezi kukiuka taratibu za utumishi bila

kushirikiana na mwanajamii katika aidha kutotenda haki au kufanya

ubadhirifu wa mali za umma.



Pamoja na Serikali kuweka utaratibu mzuri wa namna ya kushughulikia

matatizo ya utovu wa nidhamu, rushwa au ubadhirifu wa mali za umma

bado tumeendelea kushuhudia changamoto mbalimbali na nisisitize tu

kwamba serikali inaona kuna umuhimu mkubwa na haja yakuendelea

kushirikisha au kuhimiza makundi yote kwa pamoja kuhakikisha

tunaondoa tofauti na vikwazo ili kutimiza adhima iliyokusudiwa ya kumpa

mwanafunzi elimu na stadi bora, kwa kujenga misingi ya maadili

inayokubalika kitaifa na uwepo kwa ushirikiano wa pamoja.


Baada ya kusema hayo machache niiombe tu waratibu wa kampeni hii

ihakikishe inaandaa taarifa kamili na sahihi ya tathmini ya kampeni hii ya

mwezi ili yale yatakayokuwa yameibuliwa kupitia aidha vyombo vya

habari, matembezi ya hiari au Midahalo ya namna hii na yanaigusa

Serikali moja kwa moja katika mabadiliko ya Sera, Sheria, Kanuni au

taratibu tuweze kuyafanyia kazi kwa kuchukua hatua stahiki kwa wakati.

Ndugu Washiriki;

Napenda kusema kuwa kwa heshima na taadhima, sasa natamka kuwa

Mdahalo huu sasa nimeufungua rasmi.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *