Torintohot media.
Na Jerome Mlaki wa Dar. 0789106710
Maonesho ya 33 ya kimataifa ya vitabu Tanzania yamezinduliwa rasmi hii Leo na yamehudhuriwa na wananchi wengi sekta za kiserikali na zisizo za kiserikali.
Maonesho hayo yamelenga kuonyesha kazi za waandishi wa vitambu kudhamini na kutambua mchango wao ktk Taifa.
Akizungumza katika Maonesho hayo mgeni rasmi Mh. Hamis Mwinjuma Naibu Waziri wa sanaa utamaduni na Michezo amesema ili Taifa liweze kuwa na maendeleo hatuna budi kuwekeza katika kuwajengea wananchi kupenda kusoma vitabu vinavyo ongeza maarifa .
Lakini pia ameeleza vitabu vinakuza uelewa,mbali na hilo ameeleza tunakilasabu ya kuheshimu nakuitambua michango ya wazee wetu katika kuielimisha jamii kupitia usomaji wa vitabu.
Mgeni rasmi Mh Naibu Waziri Hamis Mwinjuma amesema usomaji wa vitabu unaongeza maarifa mbinu, hekima, kukuza akili na ujuzi Kwa wasomaji na hivyo tutajikuta tuna jamii yenye uelewa wa mambo mengi.
Na Kwa upande wake Hermes Damian mwenyekiti wa wachapishaji wa vitabu Tanzania, amesema kuwa Taifa ili liendelee linahiji liwekeze katika elimu na jamii inapaswa kukumbuka mchango wa wananchi waliojito katika Hali na mali katika kuandika hekima na ujuzi kwenye vitabu na Leo hii vitabu vyao vimetoa na vinaendelea kutoa mchango mkubwa wa kielimu hapa inchini.
Lakini pia Hermes Damian ameshauri kujengwe maktaba itakayo hifadhi kumbukumbu za vitambu mbalimbali vikiwemo vya wazalendo waliotoa mchanngo mkubwa Kwa Taifa katika sekta ya habari kupitia machapisho ya nalaka zao mbalimbali za vitabu hapa inchini.
Hoja ya maktaba Hermes amesema pia itatumika kama sehemu ya kuwashukuru waandishi wote wazalendo wa Taifa lao Kwa kuifadhi kazi zao vizazi na vizazi.. amesema.. usipomkumbuka mtu aliekutangulia Kwa kazi zake Bora katika Taifa.. Basi umejiandalia kaburi la kusaaulika. (Mwisho wa kunukuu)
.jpg)





0 maoni:
Chapisha Maoni