WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Ijumaa, 11 Septemba 2026

 22:32      No comments

 Na Jerome Mlaki wa Dar 0789106710.

Na Jerome Mlaki, Dar es Salaam.

Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetangaza fursa za ufadhili wa masomo nchini Algeria kwa wanafunzi 150 waliofanya vizuri katika masomo ya Sayansi kwenye mitihani ya Kidato cha Sita.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, amesema fursa hizo zimetokana na ushirikiano kati ya Tanzania na Algeria, ambapo Serikali ya Algeria italipia ada za masomo, huku Serikali ya Tanzania kupitia Samia Scholarship ikigharamia mahitaji ya kujikimu.

Prof Mkenda amesema uteuzi wa wanafunzi hao utafanyika kwa kuzingatia ufaulu bila kujali uwezo wa kifedha wa familia, hatua inayolenga kuwapa nafasi wanafunzi wenye uwezo kutoka familia za kawaida, wakiwemo watoto wa wakulima na wafugaji.

Kwa mujibu wa Profesa Mkenda, wanafunzi watakaokwenda Algeria watapewa mafunzo ya Kifaransa kwa mwaka mmoja kabla ya kuanza masomo.

Amesema wanafunzi watakaokataa nafasi hizo watabadilishwa na wanaofuata kwa ufaulu.

Ameongeza kuwa Serikali tayari imewapatia wanafunzi 10 fursa ya kusoma nchini Urusi, huku wengine 50 waliofanya vizuri katika Advanced Mathematics wakipelekwa Nelson Mandela Institute, Arusha, kwa maandalizi ya masomo ya nje mwakani.Profesa Mkenda amewataka wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo ya Sayansi kufuatilia taarifa kupitia tovuti ya Wizara na kuhakikisha simu zao zinapatikana, huku Serikali ikiendelea na mazungumzo na nchi nyingine ili kuongeza fursa za masomo ya Sayansi na Hisabati nje ya nchi.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *