Na Jerome Mlaki wa Dar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati wa hafla ya kupokea ndege mpya ya abiria aina ya Boeing 737- MAX9 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 1) Jijini Dar es salaam. (tarehe 03 Oktoba 2023)
Ndege mpya ya abiria aina ya Boeing 737- MAX9 yenye uwezo wa kubeba abiria 181 Ikimwagiwa maji (water salute) mara baada ya kuwasili nchini kwa mara ya kwanza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 1) Jijini Dar es salaam leo tarehe 03 Oktoba 2023.
Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa na viongozi mbalimbali katika picha ya pamoja na marubani na watumishi wa shirika la ndege nchini ATCL mara baada ya mapokezi ya ndege mpya ya abiria aina ya Boeing 737- MAX9 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Watumishi wa shirika la ndege nchini ATCL mara baada ya mapokezi ya ndege mpya ya abiria aina ya Boeing 737- MAX9 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikata utepe kuashiria kupokea ndege mpya ya abiria aina ya Boeing 737- MAX9 iliyowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 1) Jijini Dar es salaam leo tarehe 03 Oktoba 2023.
Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kupokea ndege mpya ya abiria aina ya Boeing 737- MAX9 katika hafla iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 1) Jijini Dar es salaam.
0 maoni:
Chapisha Maoni