Na Jerome Mlaki wa DAR
Dar es salaam:
Kampuni ya Sahara Sparks imeandaa kongamano kubwa la vijana wabunifu litakalofanyika kuanzia tarehe 18 mpaka 21 oktoba jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa wiki ya Shara Sparks, Mkurugenzi Mtendaji wa Shara Ventures, Bwana Jumanne Mtambalike amesema kongamano hilo litajadili namna gani ubunifu, teknolojia na ujasiriamali vinaweza kuwa ni chachu ya kuchangia maendeleo ya Tanzania.
"Sahara Ventures ni Kampuni tanzu ya Shara Sparks ambayo inaandaa hili kongamano la vijana wabubifu lakini velevile ambao wanajiuhusisha na masuala ya teknolojia na ujasiriamali," Alisema bw. Mtambalike,
Alisema kipindi cha takribani miaka saba (7) Sahara Ventures wamekuwa wakiandaa hili tukio la Sahara Sparks kama Jukwaa ambalo linaleta pamoja vijana wenye mawazo ya kiubunifu, lakini pia na watunga sera kuweza kujadili mnagani ubunifu, teknolojia na ujasiriamali vinaweza vikawa ni chachu ya kuchangia maendeleo ya Tanzania kama Taifa
bw. Mtambalike aliongeza kuwa katika kongamano hilo mijandala na mada mbalimbali zitawasilishwa na mwaka huu kongamano hilo limebeba kauli mbiu ya "Potantial Unleashed" kwamba namna gani wanaweza kufungua uwezo wa vijana kupitia teknolojia, ubunifu pamoja na ujasiriamali.
"Kutakuwa na mijadala mbalimbali ambayo itaanza rasmi tarehe 18 hadi 21 mada ambazo zitagusa nyanja mbalimbali na namna gani teknolojia na ubunifu vinatumika kwenye elimu, Afya, nishati na ajira," alisema bw Mtambalike.
Aidha bw. Mtambalike, aliongeza kuwa katika kongamano hilo kutakuwepo na mijadala mingi sambamba na kuvumbua fursa nyingi kwa vijana kwa kushirikiana na wadau ambao ni pamoja na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Mradi wa Funguo na Clouds Media Group.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt. Amos Nungu amesema wao kama wasimamizi wa masuala ya ubunifu, wanakila sababu ya kuhakikisha vijana wanapata fursa ya kuonekana, kubadilishana mawazo na kuweza kutangaza biashara zao.
"Ukweli ni kwamba vijana wana mawazo mazuri, kwahiyo kuwa na Jukwaa kama hili ni sehemu inayowapa fursa vijana kujitambua, kuwa pamoja na kuwa wabunifu lakini wanajua soko lina taka nini," Alisema Dkt. Nungu.
Alisema vijana wanakutanishwa na kujifunza na kukutana pia na wawekezaji wa kuweza kukuza mawazo yao. Kwasababu siku zote serikali kazi yake ni kuweka mazingira wezeshi. Serikali sio mfanyabiashara.
Aidha kupitia kongamano hili liloandaliwa na Sahara Sparks litasaidia kuwajengea zaidi vijana uwezo wa kujua lugha ya kutumia ambayo mwekezaji anaitaka
0 maoni:
Chapisha Maoni