WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumanne, 5 Juni 2018

 02:35      No comments

Image result for picha za january makamba
Jerome Mlaki
Mwambawahabari
Viongozi wa dini nchini wameihimiza jamii kujenga utamaduni wa kuyatunza na kuyahifadhi mazingira kwa ajili ya ustawi wa vizazi vilivyopo na vijavyo.

Aidha, wameiomba Serikali kusisitisha matumizi ya mifuko ya plastic ili kupunguza uharibifu wa mazingira unaosababishwa na mifuko hiyo.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam kwa wakati tofauti na viongozi wa madhehebu wa dini wakati wa Mjadala wa Kitaifa kuhusu imani ya Dini na katika kuhifadhi mazingira katika wiki ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira itakayofikia kilele Juni tano mwaka huu katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.

Akizungumza katika mjadala Padri wa Kanisa Katoliki, Raymond Saba amesema jamii inatakiwa kuvitengea haki vizazi vilivyopo na vijavyo kwa kuyatunza na kuyahifadhi mazingira na kwenda kinyume kumkosea Mungu muumba wa mazingira.

“ Tuvitendee haki vizazi hapa duniani hata Mwenyezi Mungu katika maandiko yake anaitaka jamii kuyatunza na kuyahifadhi mazingira hivyo kuyaharibu ni kumkosea,” amesema.

Amebainisha kuwa viongozi wa dini wanatakiwa kutumia miundombinu ya dini kuihimiza jamii kwa kuipa ujumbe wa utunzaji na uhifadhi mazingira.

Kwa upande wake, Askofu wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Alex Malasusa ameikumbushia Serikali kuhimiza wananchi kuacha matumizi ya mifuko hiyo  kwani inachangia uharibifu wa udongo.

Amesisitiza kuwa kanisa hilo linashiriki kampeni ya utunzaji mazingira kwa kupanda miti zaidi ya 3000 kwenye vijiji na wilaya iliyopandwa na vijana katika wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Naye Mjumbe wa Baraza la Ulamaa-Baraza la Waislamu Tanzania, Sheikh Othman Issa amesema kuna uharibifu mkubwa wa mazingira ambapo kiasi cha tani milioni nane za plastiki zinatupwa baharini hali inayohatarisha ustawi wa viumbe.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba amesema Serikali iatayafanyia kazi mapendekezo mbalimbali ya utunzaji wa mazingira yaliyaowasilishwa na viongozi.



Katika hatua nyingine, amesema Serikali iko tayari kufanya kazi na vyombo vya habari vinavyomilikiwa na taasisi za dini katika masuala ya utafiti wa mbinu za utunzaji mazingira.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *