TORINTO HOT BLOG.
Na. Jerome Mlaki
waziri wa nchi ofisi ya makamo wa rais muungano na mazingira JANUARY MAKAMBA aliyekaa katikati akifurahia jambo kulia kwake ni mkuu wa wilaya ya temeke felix Lyaviva. |
msanii wa bongo fleva chegge akiwaburudisha mashabiki katika viwanja vya mbagala zacheem. |
mashabiki wakipiga shangwe mara baada ya kuburudishwa na burudani kali ya muziki. |
mashabiki wakipiga shangwe mara baada ya kuburudishwa na burudani kali ya muziki. |
Dar es salaam
Na Jerome Mlaki
Maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es salaam na viunga vyake june 3,2018 walijitokeza kwa wingi kwenye tamasha kubwa lililolenga kutoa elimu na kuwajengea uelewa wananchi juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira.
Tamasha hilo ambalo liliandaliwa na ofisi ya makamo wa rais,muungano na mazingira pia lilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa serikali na mkoa wa Dar es salaam akiwemo Mbunge wa viti maalum [CUF]wa jimbo la Temeke ambapo maelfu ya wananchi walijitokeza ikiwa ni kupata burudani na kuunga mkono juhudi za serikali katika masuala ya utunzaji wa mazingira.
Awali akizungumza katika tamasha hilo ambalo lilirushwa live pia na kituo cha televisheni cha Clouds Tv waziri wa nchi ofisi ya makamo wa rais,muungano na mazingira JANUARY MAKAMBA amesema kuwa serikali imefurahishwa kwa kuona muitikio wa wananchi katika tamasha hilo umekuwa mkubwa huku akiendelea kuwa serikali itaendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa kutunza mazingira kwa kushirikiana na taasisi mbali zikiwemo taaasisi za kidini na mashule mbali mbali ya binasi na serikali.
''mpango huu wa kutoa elimu ya mazingira si kama utaishia tu hapa jijini Dar es salaam bali utaendelea nchi nzima na si kwa matamasha kama hili hapana ni kwa kuweka mipango madhubuti ya kushirikisha na taasisi nyingine pia zikiwemo za kidini na mashule ili kulifanya suala la utunzaji wa mazingira kama suala mtambuka kwa wananchi wote"alisema waziri Makamba
Naye mkuu wa wilaya ya Temeke FELIX LYAVIVA akizungumza katika tamasha hilo alisema yeye kama kiongozi wa wilya ya temeke na viongozi wengine wa wailaya hiyo wamerkuwa wakifanya jitihada mbali mbali ikiwemo kufanya makongamano na kuhamasisha wananchi juu ya masuala ya kutunza mazingira sambamba na kuhakikisha kunakuwepo na magari mengi ya kubebea taka kwa wakati huku akitoa wito kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam kupanda miti ya matunda ambayo itatunza mazingira na kuwaongezea vipato.
Tamasha hilo ambalo ni moja kati ya matukio yanayoendelea kuelekea kilele cha siku ya mazingira duniani may 5 mwaka huu lililofanyika katika viwanja vya Mbagala Zacheem liliwakutanisha wasanii mbali mbali kwenye jukwaa moja akwemo Chegge Chigunda,Wabantu na mkali wa visingeli anayefanya vizuri na wimbo wake wa ''mwanaume mashine''Msaga sumu ambao walifanya show kali iliyoibua shangwe kubwa kwa mashabiki zao na baadaye wananchi walipata zawadi mbali mbali ikiwemo majiko ya gesi na mkaa mbadala zawadi ambazo zilitolewa na wirara ya ofisi ya makamo wa rais,muungano na mazngira.
0 maoni:
Chapisha Maoni