Katika maadhimisho ya wiki ya Mazingira yenye kauli Mbiu mbiu 'Mkaa ni Gharama Tumia nishati Mbadala' yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazimmoja vilivyopo halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam,kampuni ya Tanzania Power Spot wamekuja na nishati ya Umeme inayozalishwa kwa kutumia mkaa ambapo inawezesha kupata Umeme.
Hii ni hali isiyo ya kawaida jiko la Mkaa linaweza kusaidia Balbu kuwaka na kuweza kupata mwanga kama ilivyo umeme wa kawaida ambapo unakuwezesha kuchaji Simu kwa kutumia Power Bank.
Akiongea na Utouh News Mkurugenzi msaidizi wa Kampuni hiyo Lukas Singili amesema kampuni hiyo inawawezesha wananchi kupata Umeme kwa kupitia Jiko la Mkaa ambapo unapika huku ukipata mwanga wa taa kutoka kwenye jiko.
"Sisi kampuni yetu inawawezesha wananchi wanaoishi maeneo ambayo umeme haujafika kuweza kupata umeme kwa kupitia majiko ya Mkaa na kupitia Mkaa mbadala" Amesema.
Aidha amebainisha kuwa matumizi ya Mkaa kuzalisha Umeme hauna madhara yoyote kwani unatumia pale unapopika hivyo hauwezi kusababisha madhara kwa watumiaji.
"Matumizi haya ya Nishati mbadala ya Umeme tunayoitengeneza hakuna Madhara yoyote kwani Waya unaotumika kupitisha moto hausababishi madhara Pia tuna imani mtumiaji atakuwa mwangalifu" Amesema Lukas.
Itakumbukwa kuwa Wiki ya Mazingira Ilizinduliwa mnamo tarehe 30 Mei 2018 na Waziri mkuu wa Tanzania Mhe. Kassimu Majaliwa na maadhimisho hayo yanatarajiwa kumalizika na kufungwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Kesho June 5, mwaka huu katika Viwanja vya Mnazimmoja Jijini hapo.
0 maoni:
Chapisha Maoni