WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Alhamisi, 2 Novemba 2017

 00:16      No comments

Dodoma. Baada ya Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kuacha kuwapangia vyuo wanafunzi, Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) kimepata ongezeko la wanafunzi kutoka 4,500 hadi 12,000 kwa mwaka wa masomo wa 2017/2018.

TCU imeacha kuwapangia wanafunzi vyuo kutokana na agizo lililotolewa na Rais John Magufuli mwaka huu, alipozindua mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Ofisa Uhusiano wa Udom, Beatrice Baltazar amesema jana Jumanne Oktoba 31,2017 kuwa, katika mwaka wa masomo wa 2016/17 walipata wanafunzi 4,500 kutoka TCU.

Amesema mwaka huu wa masomo wamepata maombi ya wanafunzi 43,000 na waliochaguliwa ni 12,000 ambao wamekidhi vigezo.

Amesema ili kudhibiti tatizo la msongamano wa wanafunzi wanaosajiliwa chuoni hapo wameboresha utaratibu kwa kuongeza watumishi wanaowasajili na huduma za benki kusogezwa chuoni.

Ofisa huyo amesema Benki ya CRDB inatoa huduma kwa kutumia tawi linalohamishika na kuwa na mawakala, hivyo wanafunzi hufungua akaunti chuoni badala ya kwenda mjini.

Meneja wa Tawi la CRDB Udom, Chabu Mishwaro amesema wameamua kusogeza huduma karibu na wanafunzi ili kupunguza usumbufu ambao

wanaupata katika mchakato wa usajili.

Mwanafunzi aliyesajiliwa katika chuo  hicho, Ikupa Mwambene amesema kusogezwa huduma kumemsaidia kutopata usumbufu wa kwenda kutafuta huduma na hatari ya kuibiwa na matapeli.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *