WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumatatu, 6 Novemba 2017

 23:34      No comments


AMA kweli elimu haina mwisho. Hilo limethibitishwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa ambaye pia ni baba wa watoto 14 mkazi wa wilaya ya Kamuli, John Bosco Mutebe anayejiandaa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi Novemba, mwaka huu.
Mutebe (44), ataungana na wanafunzi wenzake 128 wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Kyeera, Kata ya Namwendwa kufanya mitihani. Jumatano iliyopita, baba huyo wa mabinti 11 na watoto watatu wa kiume ambaye ni kiongozi Kanda ya Bwaguusa, alishiriki ibada maalumu ya kuombea wanafunzi wa darasa la saba iliyofanyika Kanisa Katoliki Namwendwa na kuongozwa na Padri Fredrick Wobeera.
Mutebe ambaye pia ni Katekista katika mji mdogo Ngandho wilayani Buyende, alienda shuleni Februari mwaka huu akiomba aruhusiwe kufanya mtihani wa darasa la saba baada ya kukatisha masomo darasa la sita mwaka 1989. Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Sam Caleb Opio anasema: “Kwa kuwa ni kiongozi wa eneo hili, tulijua ana ziara ya kawaida. Lakini alishangaza kusema anataka kurudia darasa la saba.”
Mutebe alisema kutokana na kukosa sifa za kielimu, amekosa nafasi nyingi kanisani na ajira katika mashirika yasiyo ya Serikali huku akikiri anajiona amefanya makosa akiwa madarakani, sababu kubwa ikiwa kukosa elimu ya kutosha.
“Ninaheshimika na nina uelewa mkubwa wa mambo, ndiyo maana ninashikilia ofisi ya umma, lakini siku zote nimekuwa nikijisikia vibaya kutokana na elimu duni,” alisema Mutebe anayeamini atafaulu na kuingia kidato cha kwanza mwakani akiapa kusoma kwa bidii na hatimaye awe mtaalamu wa kilimo kwa kuwa tayari ni mkulima na anapenda kilimo.
Akiwa mwenye furaha, anasema anashukuru kutimiza ndoto ya kuhitimu darasa la saba, jambo ambalo kwa wengi lilionekana sawa na ndoto hasa kwa kuwa tayari ana familia kubwa. Mwalimu wa darasa analosoma Mutebe, Francis Balimisa Kapere, amesifu juhudi na nidhamu yake akisema licha ya umri na hadhi yake kama kiongozi wa Serikali, ni mtaratibu, msikivu, ana uwezo mkubwa darasani na hakosi vipindi.
Wanafunzi wanzake wamemwelezea kuwa ni mtu anayejituma katika masomo na kwamba anawazidi wengi kwa uwezo wa darasani. Mama mzazi wa Mutebe, Rosemary Nantume, anasema kama si ulevi wa baba yake kiasi cha kumfanya akose ada za watoto, mwanaye huyo angefika mbali kielimu, lakini kutokana na mazingira ya familia, alikatisha masomo yake.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *