Na Torinto Manuver Dar
Dokta mkuu wa Taasisi ya Aga Khan Dk. Lucy kway wa katikati akizungumza na vyombo vya habari kuhusu kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika matembezi hayo.(Picha zote na mpiga picha wetu Utouh News)
Na Torinto Manuver-Dar
Vifo vitokanavyo na saratani ya matiti vinategemea kuongezeka na kufikia milioni 24 ifikapo mwaka 2035 kama juhudi za kuzuia na tiba hazitaimarishwa katika nchi zenye uchumi wa kati.
mpaka sasa tatizo la saratani limekuwa likiongezeka siku hadi siku duniani kote na hasa katika nchi zinazoendelea kama Tanzania huku takwimu zilizotolewa na Shirika la Afya duniani (WHO) zikionyesha ongezeko la wagonjwa wapya 14.1 milioni hugundulika kila mwaka huku na wagonjwa 8.8 hufariki.
akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk Julius Mwaiselage alisema athari za kiuchumi zitokanazo na ugonjwa wa saratani ni kubwa na zinaongezeka kila mwaka ambapo mwaka 2010 zilikadiliwa kufikia dola za kimarekani trilioni 1.16 kila mwaka.
"Takwimu duniani kote saratani ya matiti ndiyo iliyoongoza kwa kuwa na wagonjwa wapya milioni 1.7 kila mwaka wanagundulika ikilinganishwa na wagonjwa laki 5 wanaogundulika na saratani ya shingo ya kizazi," alisema Mwaiselage
Na kuomgeza kuwa "lakini ieleweke kuwa saratani ya mlangi wa kizazi ndiyo inayoongoza kwa kuwa na asilimia 35-40 ya wagonjwa wote huku saratani ya matiti ni asilimia 10-15," aliongeza.
mbali na kuwepo kwa ongezeko la wagonjwa hao taasisi ya saratani ya ocean road kw kushirikiana na hoteli ya Kunduchi beach na Hospitali ya Agha Khan imeandaa matembezi ya hisani yatakayofanyika kesho Oktoba 28 2017 na kuhudhuriwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto, Ummy Mwalimu.
matembezi hayo yatafanyika kuanzia taasisi ya saratani ya oceaan road saa 12:30 asubuhi na kuhitimishwa saa 4:00 asubuhi katika taasisi ya hiyo na lengo matembezi hayo ni kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu saratani ya matiti.
kwa upande wake mkurugenzi wa wauguzi kutoka hospitali ya Agha khan,Dk. Lucy kway alisema kuwa hospitali hiyo imekuwa ikiungana na taasisi ya ocean road katika kutokomeza magonjwa ya saratani.
"Kwa kufanikisha kutolewa kwa elimu juu ya saratani na upimaji wa bure wa ugonjwa huo kila jumamosi ya mwisho wa mwezi tunatoa elimu kupitia madaktari bingwa kutoka katika hospitali yetu hivyo wadau mbalimbali wajitokeze kushiriki na kuchangia katika kampeni ya kutokomeza saratani," alisema dk kway
0 maoni:
Chapisha Maoni