Na Neema Sudai wa Torinto Hot Blog.
Benki ya biashara na maendeleo mashariki na kusini mwa afrika maalufu kama TPA imebadili rasmi jina la biashara Leo na kuanza kutumia jina la TDB.
Hayo yamesemwa Leo na Afisa mkuu mtendaji wa benki hiyo Admassu Tadesse alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuwa benki hiyo kuanzia 31 October itakuwa ikitumia jina la benki ya biashara na maendeleo Trade and Development Bank TDB ikiambatana na nembo mpya ya jina hilo.
Aidha Tadesse amesema jina la usajili kisheria la benki ya biashara na maendeleo mashariki na kusini litabaki kama lilivyo na kuongeza kuwa itaendelea kuwezesha utekelezaji wa miradi iliyopo kwenye sekta zitakazopewa kipaumbele kama vile miundo mbinu,viwanda na biashara ya kilimo miongoni mwa nchi 21 inamofanyia shughuli zake katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Hata hivyo Tadesse amesema usanifu wa jina letu unaashiria kuwa wameibuka na nguvu mpya na dhamira mpya katika kuimarisha biashara,maendeleo ya uchumi na ushirikiano wa kikanda katika kipindi ambacho ukanda mzima ambapo umeinua kwa dhati kusukuma mbele mageuzi ya kiuchumi na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi.
Pia Tadesse ameongeza kuwa kubadili jina kumekuja baada ya miaka kadhaa kupita ambapo kwa kipindi chote kumeongezeka ubora wa Mali na faida pamoja na ubunifu inayofanya benki hiyo kuwa ya kisasa zaidi.
Endeleo Kufuatilia Torinto Hot Blog.
0 maoni:
Chapisha Maoni