Diterbitkan 12:12:00 PM
TAGS
Rais Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Mwanza katika mkutano wa hadhara ikiwa ni moja ya vitu alivyopanga kuvifanya katika ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani hapo.
Ameeleza kuwa ameona ni sahihi kuanza na mambo ya muhimu zaidi kama vile miundombinu ya barabara, huduma za afya pamoja na elimu kabla ya kutoa fedha hizo ambazo aliziahidi katika iilani ya uchaguzi wa mwaka 2015.
“Halitokuwa jambo jema mimi kutoa milioni 50 kwa kila kijiji nchini wakati huduma mbalimbali kama vile elimu, afya na miundombinu ya barabara na usafirishaji haijakaa vizuri. lakini niwahakikishie kuwa hizo fedha zipo na zitakabidhiwa kwa kila kijiji kama nilivyosema,” alisema Rais Magufuli.
“Inabidi muwe watulivu wakati serikali ikishughulikia matatizo na changamoto zinazohitaji utatuzi wa haraka kabla hatujazitoa fedha hizo,” aliongeza Rais Magufuli.
Rais Magufuli alimtaka pia Mkuu wa mkoa wa mwanza kuhakikisha kuwa anachochea maendeleo ya viwanda na kupitia hivyo nchi itapata maendeleo.
“Viwanda vitatengeneza ajira nyingi kwa watanzania na vitaongeza mapato ya serikali. Mapato yakiongezeka serikali itaweza kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi,” Alisema Rais.
0 maoni:
Chapisha Maoni