WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumanne, 10 Oktoba 2017

 04:14      No comments


 TAGS

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Nyakoro Sirro amefunguka na kusema kuwa jeshi la polisi linatambua makosa ya kimtandao yanayofanywa na mwanadada Mange Kimambi na kusema kuwa jeshi la polisi linashughulikia suala hilo.

IGP Sirro mesema hayo jana  alipokuwa mjini Iringa kwenye ziara ambapo alisema kuwa jeshi la polisi linatambua uvunjifu wa sheria ya makosa ya kimtandao yanayofanywa na mwadada huyo maarufu mitandaoni ambaye amekuwa mkosoaji wa mambo mbalimbali na kutoa machapisho ambayo serikali inaona ni ya matusi na kashfa kwa serikali na viongozi wake.

Aidha IGP Sirro alisema kuwa kwa sasa hawawezi kuweka wazi ni hatua gani zinachukuliwa dhidi ya mwanadada huyo ambaye kwa sasa anaishi nchini Marekani

Mbali na hilo  IGP Sirro alisema jeshi hilo halitawavumilia maafisa wa polisi na askari wanaowasaidia watu wanaofanya unyanyasaji kwa watoto kwa kuwafanyia vitendo vya ubakaji na ulawiti ili kukwepa mkono wa sheria huku akiwataka wananchi wanaohisi kutotendewa haki katika kushughulikia makosa ya aina hiyo kupeleke malalamiko kwa wakuu wa mikoa na viongozi wengine.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *