WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumanne, 10 Oktoba 2017

 04:33      No comments


 TAGS
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai, amewataka mawaziri wapya walioapishwa hapo jana Oktoba 9 kujiandaa kuchapa kazi kwa nguvu zote, kwani wakati uliopo sio wa kuzembea.

Kauli hiyo ya Ndugai ameitoa jana alipokuwa akiwapongeza Mawaziri hao, ambao awali wengine walikuwa wabunge wa kawaida na sasa kuveshwa kofia za uwaziri, na kwamba wakienda bungeni ni kuchapa kazi kwani walishapata uzoefu miaka miwili iliyopita tangu awamu ya tano iingie madarakani.

"Mheshimiwa Rais ni matumaini ya watanzania kwamba timu hii ambayo inaimarisha Baraza la Mawaziri, na kama tulivyoambiwa hapa wanaanza kazi leo leo kwa kikao cha Baraza la Mawaziri, tunawatakia kila la heri, tunawakiribisheni bungeni, niwaambie neno moja tu mbele yako Mheshimiwa Rais wajiandae, hawa walioapishwa na hawa wengine waliokuwepo, hii miaka miwili ya mwanzo tulikuwa tunachukulia wanajifunza, sasa hivi tukienda Dodoma ni kazi tu", amesema Spika Ndugai.

Hapo Jana Rais Magufuli ameapisha Baraza la Mawaziri baada ya kulifanyia mabadiliko Oktoba 7, na kuwataka waanze kazi mara moja, huku wakikabidhiana nyaraka za ofisi tayari kwa utekelezaji.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *