WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumanne, 25 Julai 2017

 00:03      No comments


 TAGS
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg
Shaka Hamdu Shaka (MNEC)akizungumza wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM, katika ukumbi Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela
Kaimu
Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg
Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akikagua mradi wa vijana wa umwagiliaji Mtaa wa Imalang’ombe wakati wa ziara ake ya kikazi Katika Manispaa ya Ilemela

 Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Manispa ya Ilemela pamoja na Wageni toka nchini Sweeden wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg
Shaka Hamdu Shaka (MNEC katika ukumbi wa mikutano Halmashauri ya Wilaya ya ilemela

 Kaimu
Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg
Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akishiriki shughuli ya ufyatuaji tofali kuwaunga mkono vijana wa kikundi kinachodhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Anjeine Mabula

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Ilemela Kheri D Jemes  (wa pilikulia)akitoa ufafanuzi katiaka mradi wa vijana wa kufyatua matofali katiak  kikundi kinachodhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Anjeine Mabula


  Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg
Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akizungumza na vikundi vya wajasiliamali Vjana na kinamama vilivyo nufaika na pesa ya Asilimia 5 kwa vijana na kinamama wilayani ilemela .

 Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg
Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akifungua rasmi ofisi ya vijana wajasilia mali walionufaika na fedha za asilimia 5 za vikundi katika halmashauri ya wilaya ya ilemela.

 Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg
Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akizindua Shina la wakereketwa wa Chama cha Mapinduzi katika eneo la Nyehunge

 Shina lililozinduliwa na  Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg
Shaka Hamdu Shaka (MNEC alipokutana kuzungumza na viongozi na wanachama wa ccm katika Uwanja wa CCM KIRUMBA.

 Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg
Shaka Hamdu Shaka (MNEC) wa pili kulia akivikwa Stafu na Moja wa GREEN GUARD  alipokutana kuzungumza na viongozi na wanachama wa ccm katika Uwanja wa CCM KIRUMBA.

 Wanachama na Viongozi wakipunga mikono
 Mhe Mbunge wa jimbo la ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi akizungumza wakati wa mkutano wa ndani waKaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg
Shaka Hamdu Shaka (MNEC alipokutana kuzungumza na viongozi na wanachama wa ccm katika Uwanja wa CCM KIRUMBA.

Katibu wa Mkoa wa CCM ndg:akizungumza wakati wa mkutano wa ndani wa Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg
Shaka Hamdu Shaka (MNEC alipokutana kuzungumza na viongozi na wanachama wa ccm katika Uwanja wa CCM KIRUMBA
.
  (PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI )

Na Mwandishi Wetu, Mwanza


Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa
umetangaza kiama dhidi ya Halmashauri zote nchini zisizotoa asilimia 5
ya mikopo kwa Vijana kama ilivyoainishwa na Ilani ya Ushindi wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM).


Umoja huo umesema kuwa hakuna Taifa lolote Duniani ambalo
linaweza kuajiri Vijana wote badala yake Vijana husaidiwa na Serikali
kupitia mbinu Mbalimbali za kuwakwamua kiuchumi ikiwemo kuwapatia mikopo
na kuwasaidia kujiajiri.


Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg
Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Leo Julai 24, 2017 Wilayani Ilemela Mkoani
Mwanza Wakati wa ziara ya siku moja alipokuwa akizungumza na Vijana wa
Jumuiya ya Chama hicho (UVCCM) pamoja na  wanachama wa chama cha
Mapinduzi (CCM) katika mkutano wa ndani uliofanyika katika Uwanja wa CCM
Kirumba.


Shaka alisema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinafahamu
kuwa Changamoto kubwa ya Vijana nchini ni ukosefu wa ajira lakini
Serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi inaendelea kutumia njia
Mbalimbali ikiwemo kuwashauri Vijana Kujiunga na vikundi Mbalimbali ili
wapatiwe mikopo waweze kujiajiri wenyewe.


“Nitakuwa muongo kama nitasema sifahamu changamoto
zinazowakabili Vijana wengi kiuchumi kwa wale waliopo ndani ya Chama Cha
Mapinduzi ama wale waliopo nje ya CCM lakini Serikali inayotekeleza
ilani yetu ya ushindi ya Mwaka  2015 imeeleza vyema namna bora ya
kuwasaidia Vijana kujiajiri” Alisema Shaka


Alisema kuwa Vijana na watanzania kwa ujumla wake wanapaswa
kujituma kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuunga mkono juhudi za Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli za kuwaletea
maendeleo huku akisifu Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kwa kuanza
vyema kuwapatia mikopp Vijana wa Manispaa hiyo.


Alisisitiza kuwa Vijana wanapaswa kuanzisha vikundi vya
ujasiriamali, na Vikundi vya uzalishaji Mali, Vitakavyowasaidia wao
Vijana, Wanawake na Taifa kwa ujumla kupambana na hali ya kiuchumi
katika jamii.


Shaka amewasihi Vijana kurudisha haraka fedha za mikopo
pindi wamalizapo matumizi ya fedha hizo ili ziweze kuwasaidia Vijana
wengine, zaidi amewasihi Vijana wote kuwa wabunifu kwenye kipato ili
waweze kuishawishi Serikali kuwaongeza fedha nyingi katika miradi yao.


Sambamba na hayo pia Shaka amesifu Ofisi ya Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la
Ilemela,  sambamba na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa kazi kubwa ya
kuwashirikisha Vijana katika shughuli za maendeleo wanazozifanya.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *