WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumatatu, 3 Julai 2017

 01:50      No comments
Habarini za asubuhi,

Haya ndiyo yaliyojiri kwenye soko la hisa wiki iliyoisha Ijumaa tarehe 30 Juni 2017.

Mauzo ya Hisa (Turnover/ Liquidity)

Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imepungua kutoka hisa milioni 2.39 wiki iliyoisha tarehe

23 Juni 2017, hadi hisa 335,000 kwa wiki iliyoishia 30 June 2017. Hivyo pia thamani ya mauzo ya

hisa kupungua kutoka Shilingi bilion 19 wiki iliyopita hadi Shilingi milioni 412 wiki hii iliyoishia

tarehe 30 Juni 2017.

Kampuni zilizoongoza katika mauzo ya hisa ni kama ifuatavyo:

TCC …………………………………………..……70.41%

CRDB ……..…….………………..…………..………11.86%

TBL …….....……..……….…………....………… 7.97%

Ukubwa Mtaji (Market Capitalization)

Ukubwa wa mtaji wa kampuni zilizoorodheshwa katika soko umepanda kwa Shilingi Bilioni 438

kutoka Shilingi Trilioni 18.8 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 19.2 wiki iliyoishia tarehe 30 Juni

2017. Hii ni kutokana na kupanda kwa bei za hisa za USL (15.38%), TCC (12.76%) na KA (7.14%).

Ukubwa wa mtaji wa kampuni za ndani umepanda kwa Shilingi Bilioni 124 kutoka Shilingi

Trilioni 7.6 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 7.75 wiki hii. Hii ni kutokana na kupanda kwa bei ya

hisa za TCC (12.76%).

Hati Fungani (Bonds)

Mauzo ya hati fungani katika wiki iliyoishia tarehe 30 Juni 2017 yamepanda kutoka Shilingi

milioni 770 wiki iliyopita hadi Shilingi Bilioni 9.6

mauzo haya yalitokana na hatifungani nne (4) za serikali na za Makampuni zenye jumla ya

thamani ya Shilingi bilioni 11.04 kwa jumla ya gharama ya Shilingi Bilioni 9.6.

Viashiria (Indices)

Kiashiria cha kampuni zilizoorodheshwa katika soko yaani DSEI kimepanda kwa pointi 40 kutoka

pointi 2,127 hadi pointi 2,166 kutokana na kuongezeka kwa bei za hisa za kampuni mbali mbali

zilizopo sokoni.

Kufuatia kupanda kwa bei za hisa, kishiria cha kampuni za ndani yaani TSI kimepanda kwa pointi

59 kutoka pointi 3,632 wiki iliyopita hadi pointi 3692 wiki hii.

Kiashiria cha sekta ya viwanda (IA) imepanda kwa pointi 110 kutoka pointi 4,803 wiki iliyopita

hadi pointi 4914 wiki hii kutokana kupanda kwa bei za hisa za TCC kwa 12.76% kutoka Shillingi

9800 hadi 11,050.

Kiasharia cha huduma za kibenki na kifedha (BI) wiki hii kimepungua kwa pointi 0.6 kutoka

pointi 2,515 hadi pointi 2,514.64 kutokana na ongezeko la bei ya hisa za DSE (1.69%)

Kiashiria cha Sekta ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii imebaki kwenye wastani wa 2,467

kama awali.

Shindano la Wanafunzi la Uwekezaji

Shindano la DSE SCHOLAR INVESTMENT CHALLENGE 2017 lilifika mwisho tarehe 30 Juni 2017.

Zaidi ya wanafunzi wa vyuo na secondary 11,000 walishiriki katika shindano la mwaka huu,

ikiwa ni Zaidi ya mara 3 ya mwaka uliopita, 2016.

Matokea ya washindi wa shindano hili yatatangazwa tarehe 10 July zoezi la uchambuzi litakapo

anza.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *