WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumatatu, 5 Juni 2017

 05:43      No comments


  • Saa 2 zilizopita
Mji mkuu wa Qatar, DohaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMji mkuu wa Qatar, Doha
Mataifa sita ya Kiarabu, zikiwemo Saudi Arabia, Misri, Bahrain, Umoja wa Milki za Kiarabu na Yemen, yamekata uhusiano wao wa kidiplomasia na Qatar yakiilaumu kwa kuvuruga uthabiti katika eneo hilo.
Nchi hizo zimeilaumu Qatar kwa kuunga mkono makundi ya kigaidi, likiwemo kundi la Islamic State (IS).
Shirika moja nchini Saudi Arabia linasema kuwa taifa hilo limefunga mipaka yake na kusitisha usafiri wa ardhini, baharini na angani.
Lilinukuu maafisa wa Saudia wakisema kuwa hatua hiyo ni ya kulinda usalama wa nchi kutokana na hatari za ugaidi na itikadi kali.
Kile ambacho kwa wiki kadhaa kimekuwa kikichochea mzozo baina ya mataifa ya Ghuba sasa kimelipuka kuwa mzozo kamili wa kidiplomasia.
Katika tangazo la pamoja, Saudi Arabia ilikuwa ya kwanza kusema kuwa inavunja mahusiano yake ya Qatar mapema Jumatatu , mara moja ikafuatiwa na Bahrain, Muungano wa Milki za kiarabu Misri na Yemen.
Hatua za kwanza za mzozo huu zilionekana kujitokeza mwezi Mei wakati Qatar iliposema shirika lake rasmi la habari lilidukuliwa pamoja na kauli ambayo haikuwa sahihi iliyosemekana kutolewa na mtawala wake, iliyoonekana kwenye mtandao ikisifu kundi la wanawamgambo wa Iran na Lebanon la Hezbollah.

Taifa la Qatar

Mji Mkuu: Doha

  • 2.7 milioni Idadi ya watu
  • 11,437 sq km Ukubwa wa eneo
  • Kiarabu Lugha
  • Kiislamu Dini
  • 78.5 Umri wa watu kuishi
  • Riyal Sarafu
Getty Images
Misri nayo imefunga anga zake na bandari kwa Qatar, kwa mujibu wa wizara ya mashauri ya nchi kigeni.,
Milki ya nchi za kiarabu imewapa wanadiplomasia wa Qatar saa 48 kuondoka nchini humo.
Rais wa Marekani Donald Trump alikutana na Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi (kushoto) na Mfalme Salman wa Saudi Arabia nchini Saudia wiki mbili zilizopitaHaki miliki ya pichaEPA
Image captionRais wa Marekani Donald Trump alikutana na Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi (kushoto) na Mfalme Salman wa Saudi Arabia nchini Saudia wiki mbili zilizopita
Abu Dhabi inaishutumu Qatar kwa kufadhili ugaidi na itikadi kali.
Shirila la taifa la habari nchini Bahrain nalo limesema kuwa nchi hiyo inataka uhusiano na Qatar kwa kuvuruga usalama wake na kuingilia ndani masuala yake ya ndani.
Qatar na nchi nyingine za Ghuba

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *