VITAMBULISHO VYA TAIFA BUNGENI VYATOLEWA KWA WABUNGE MJINI DODOMA
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano (NIDA) Bi. Rose Mdami, akimkabidhi Kitambulisho chake Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki, Mbunge wa Maswa Magharibi alipofika kuchukua kitambulisho chake leo Dodoma.
Mhe. Peter Msigwa Mbunge wa Iringa Mjini, akikabidhiwa Kitambulisho chake leo bungeni na Afisa Usajili mkoa wa Dodoma Ndg. Khalid Mrisho.
Mhe. Leonidas Gama, Mbunge wa Songea mjini, akisaini kitabu kuthibitisha kukabidhiwa Kitambulisho chake cha Taifa leo Dodoma.
Akikagua orodha yenye majina ni Mh. Yahaya Omary Massare Mbunge wa Manyoni Magharibi, wakati alipofika kuchukua kitambulisho chake cha Taifa Bungeni Dodoma leo. Kulia ni Ndg. Khalid Mrisho Afisa Usajili mkoa wa Dodoma.
Mh. Mariam Nassoro Kisangi (Mwenye kilemba kulia), Mbunge wa Viti Maalumu akipata maelezo ya kitambulisho chake kipya toka kwa Bi. Rose Mdami Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano NIDA.
……
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeanza zoezi la Ugawaji Vitambulisho vya Taifa vipya kwa waheshimiwa Wabunge wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wanaondelea na kikao chao mjini Dodoma.
Pamoja na kugawa Vitambulisho, NIDA inaendelea kuwasajili waheshimiwa Wabunge ambao hawakusajiliwa awali. Lengo ni kuhakikisha Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wana Vitambulisho vya Taifa na kuvitumia kwenye shughuli mbalimbali za utambuzi hususani kwenye Taasisi na makampuni binafsi yenye kutoa huduma kulingana na teknolojia itakavyoruhusu.
0 maoni:
Chapisha Maoni