WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumanne, 7 Februari 2017

 01:23      No comments

NA Torinto Hot Media Blog
WANACHAMA cha wananchi (CUF) wametakiwa kutoutumia mgogoro unaoendelea ndani ya Chama hicho ili kuvunja muungano uliopo kati ya Tanganyika na Zanzibar.
Ushauri huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa chama hicho ambaye anatambulika na ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa nchini,Profesa Ibrahimu Lipumba wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Ambapo Profesa Lipumba amesema inasikitisha kuona wako baadhi ya viongozi wa chama hicho wanautumia mgogoro wa kikatiba unaendelea ndani ya chama hicho ili kuharibu muungano uliopo jambo analodai halifai kufanywa na viongozi wa chama hicho kikuu cha Upinzani visiwani Zanzibar.
“Kukweli ukitoa Chama cha Mapinduzi (CCM) chama kingine ambacho kinauenzi muungano ni Chama cha CUF,hivyo nashangaa wapo viongozi wanaobeza muungano huu,hivyo lazima tuwapinge watu hawa’amesema Profesa Lipumba.
Hata Hivyo,Lipumba ameendelea kumsihi katibu mkuu wa Chama hicho,Maalim Seif kurejea ofisini ili waweze kukijenga chama hicho.
Amesema kitendo cha Katibu mkuu huyo kutokuja ofisini kunazidi kiweka vibaya chama hicho na kushindwa kueleweka kwa jamii jambo analomsihi katibu mkuu huyo kutafakari uamuzi wake wakutokuja ofisini

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *