Jumanne, 14 Februari 2017
Meya wa jiji la Der es Salaam amewaomba wazazi wenye watoto katika shule za msingi na Sekondari kushirikiana na walimu ilikusaidia wanafunzi kuweza kuwa na maendeleo mazuri kimasomo.
Akiongea na mwandishi wa habari wa TORINTO HOT MEDIA BLOG hii leo mapema ofisini kwake Mh. Isaya Mwita amesema ili wanafunzi waweze kufanya vizuri shuleni haina budi wazazi kushirikiana na walimu kikamilifu ili kusaidia mwanafunzi kuwa na maelendeleo mazuri kimasomo.
Mh. Meya amesem baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwashutumu au kuwalaumu walimu kwa kuwaadhibu wanafunzi, hata kama wanafunzi hao wamekosea, jambo ambalo Mh. Meya amesema sio sahihi badala yake wazazi wanapaswa kushirikiana na walimu kwa kuwakanya watoto kujihusisha na tabia mbaya kama uvutaji wa bangi utoro ili waweze kuwa watoto bora na wenye utii wa walimu na wazazi pia.
Aidha Mh. Meya amewaomba wazazi wasiwanunulie watoto simu kwa sababu wanafunzi bado hawajui matumizi sahihi ya simu Mh. Meya amesema kuwa, wanafunzi wengi muda mwingi hupendelea kuchati hata wakati wakiwa darasani jambo ambalo amedai huwaondolea umakini wa kufuatilia masomo.
Mh. Meya amesema kuwa, ili mwanafunzi aweze kufanya vizuri kimasomo anapaswa kufuatilia vizuri masomo na kujihusisha na shughuli mbalimbali za shuleni. Na kwa upande wa Wazazi wanapaswa kumfuatilia mtoto na kujua mienendo ya mtoto ikiwa ni pamoja uhudhuriaji wa vipindi na wazazi washirikiane na walimu wa shule husika anayosoma mtoto.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 maoni:
Chapisha Maoni