WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Ijumaa, 20 Novemba 2026

 03:32      No comments





Na. Jerome Mlaki wa Dar Es Salaam.


Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, amewaalika wawekezaji, wadau wa tiba asili na sekta ya afya kushiriki katika dhifa ya uwekezaji wa tiba asili ijulikanayo kama Asili Investment Gala 2027, inayotarajiwa kufanyika Aprili 2027, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuendeleza tiba asili na kuhakikisha inatambulika na kuunganishwa katika mfumo rasmi wa huduma za afya nchini.

Dhifa hiyo yenye kauli mbiu “Wekeza katika Dawa Zetu za Ndani za Tiba Asili” inalenga kuhamasisha uwekezaji na ushirikiano wa wadau katika uzalishaji wa dawa za tiba asili, tafiti, ubunifu na ujenzi wa uwezo wa rasilimali watu, ili kuendeleza sekta hiyo na kuongeza mchango wake katika huduma za afya.

Akizungumza na waandishi wa habari Novemba 19, 2026 Jijini Dar es Salaam, Mhe. Mchengerwa amesema Serikali inaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha tiba asili inajumuishwa katika mfumo rasmi wa huduma za afya kufikia mwaka 2030, ikiwemo huduma za afya ya msingi na mipango ya Bima ya Afya kwa Wote, kwa kuzingatia sera, miongozo na taratibu zinazotumika nchini.

Amewataka wawekezaji na wadau mbalimbali kutumia fursa ya Asili Investment Gala kujitokeza, kushirikiana na kuwekeza katika sekta hiyo, huku akiwahimiza waganga na wadau wa tiba asili ambao hawajasajiliwa kukamilisha usajili wao mapema ili waweze kutambuliwa na kushiriki katika fursa za maendeleo ya sekta hiyo.

Aidha, amesema usajili na uthibitishaji wa dawa za tiba asili ni muhimu katika kuhakikisha ubora, usalama na ufanisi wa bidhaa, kwa kushirikiana na taasisi zinazohusika na udhibiti na usimamizi wa huduma za afya, ikiwemo TMDA, MSD na taasisi nyingine zilizo chini ya Wizara ya Afya.

Kupitia dhifa hiyo, Wizara inalenga kujenga mazingira wezeshi ya uwekezaji na ushirikiano yatakayochochea maendeleo ya tiba asili, kuimarisha tafiti na ubunifu,



Dhifa hiyo yenye kauli mbiu “Wekeza katika Dawa Zetu za Ndani za Tiba Asili” inalenga kuhamasisha uwekezaji na ushirikiano wa wadau katika uzalishaji wa dawa za tiba asili, tafiti, ubunifu na ujenzi wa uwezo wa rasilimali watu, ili kuendeleza sekta hiyo na kuongeza mchango wake katika huduma za afya.

Akizungumza na waandishi wa habari Novemba 19, 2026, Mchengerwa amesema Serikali inaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha tiba asili inajumuishwa katika mfumo rasmi wa huduma za afya, ikiwemo huduma za afya ya msingi na mipango ya Bima ya Afya kwa Wote, kwa kuzingatia sera, miongozo na taratibu zinazotumika nchini.

Amewataka wawekezaji na wadau mbalimbali kutumia fursa ya Asili Investment Gala kujitokeza, kushirikiana na kuwekeza katika sekta hiyo, huku akiwahimiza waganga na wadau wa tiba asili ambao hawajasajiliwa kukamilisha usajili wao mapema ili waweze kutambuliwa na kushiriki katika fursa za maendeleo ya sekta hiyo.

Aidha, amesema usajili na uthibitishaji wa dawa za tiba asili ni muhimu katika kuhakikisha ubora, usalama na ufanisi wa bidhaa, kwa kushirikiana na taasisi zinazohusika na udhibiti na usimamizi wa huduma za afya, ikiwemo TMDA, MSD na taasisi nyingine zilizo chini ya Wizara ya Afya.

Kupitia dhifa hiyo, Wizara inalenga kujenga mazingira wezeshi ya uwekezaji na ushirikiano yatakayochochea maendeleo ya tiba asili, kuimarisha tafiti na ubunifu, pamoja na kuhakikisha tiba asili inapata nafasi katika mfumo rasmi wa huduma za afya kwa manufaa ya wananchi.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *