WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumanne, 10 Novemba 2026

 03:15      No comments

Na Jerome Mlaki wa Dar 0789106710.


Serikali ya Tanzania imeeleza dhamira yake ya kuimarisha sekta ya utalii kupitia ushirikiano na Serikali ya Italia, kwa lengo la kuongeza ubora wa mafunzo, kujenga uwezo wa wataalamu na kuongeza ushindani wa sekta hiyo ndani na nje ya nchi.


Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa programu ya ushirikiano wa mafunzo katika sekta ya utalii, mwakilishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii amesema programu hiyo ni fursa muhimu kwa taasisi za mafunzo ya utalii kuimarisha viwango vya elimu, kubadilishana uzoefu na kujifunza mbinu bora za kimataifa.



Amesema utalii ni miongoni mwa nguzo muhimu za uchumi wa Tanzania, hivyo uwekezaji katika mafunzo na maendeleo ya rasilimali watu ni hatua muhimu katika kukuza ushindani na ubora wa huduma zinazotolewa kwa wageni.


Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi za mafunzo ya utalii za Tanzania Bara na Zanzibar ili kuhakikisha manufaa ya programu hiyo yanawafikia wadau wengi zaidi katika sekta ya utalii na huduma za ukarimu.


Kwa upande wake, ametoa shukrani kwa Serikali ya Italia kupitia Shirika la Italia la Ushirikiano wa Maendeleo (AICS) kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kuendeleza programu zinazolenga kuboresha elimu na mafunzo ya utalii.


Amesema ushirikiano huo utatoa fursa ya kubadilishana maarifa, uzoefu wa kitaasisi na kutambua maeneo mapya ya ushirikiano yatakayosaidia kukuza sekta ya utalii nchini.



Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Serikali ya Tanzania, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Serikali ya Italia, Shirika la AICS pamoja na wadau wa sekta ya utalii na taasisi za mafunzo.


Mwisho, amewakaribisha washiriki wote na kueleza matumaini yake kuwa programu hiyo itakuwa chachu ya kuimarisha ubora wa mafunzo na maendeleo endelevu ya sekta ya utalii nchini Tanzania.



0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *