WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumanne, 20 Oktoba 2026

 04:03      No comments

 Serikali imeeleza umuhimu wa kuimarisha sera na mazingira ya biashara kwa kampuni changa za ubunifu (startups), huku wadau wakitaja upatikanaji wa mitaji, masoko na changamoto za kanuni za uendeshaji kuwa miongoni mwa vikwazo vinavyohitaji ufumbuzi.


Hoja hizo zimeibuliwa katika Tanzania Startup Week 2026, inayofanyika Dar es Salaam, ambapo viongozi wa Serikali na wadau wa sekta ya ubunifu wamejadili namna ya kukuza kampuni changa na kuwezesha mawazo ya vijana kugeuka biashara zenye uwezo wa kukua.


Akizungumza katika mkutano huo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, amezungumzia umuhimu wa uundwaji wa sera zitakazosaidia kuimarisha mfumo wa startups nchini na kuweka mazingira yatakayowezesha sekta hiyo kuchangia maendeleo ya uchumi.


Kwa upande wake, Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, amesisitiza umuhimu wa kuboresha mazingira ya biashara, kurahisisha mifumo ya kiutendaji na kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi ili kusaidia biashara kukua.


Kapinga amesema taasisi na wizara zinapaswa kutathmini mifumo yao, taratibu na sheria ili kubaini maeneo yanayohitaji maboresho. Lengo ni kuwezesha wafanyabiashara kupata maelekezo yanayoeleweka kuhusu huduma wanazohitaji bila kukwama kutokana na mifumo isiyoratibiwa vizuri.


Ameeleza pia kuwa Serikali iko tayari kushirikiana na wadau wa sekta binafsi katika kuendeleza biashara na kupanua masoko, huku vijana wakihimizwa kutafuta fursa za uwezeshaji zinazoweza kusaidia kukuza miradi yao.


Naye Mtendaji Mkuu wa Tanzania Startup Association, Zahoro Muhaji, ameeleza kuwa kampuni changa zinakabiliwa na changamoto zinazohusiana na upatikanaji wa fedha, masoko na kanuni za biashara, akisisitiza umuhimu wa majadiliano hayo kuzaa hatua za utekelezaji.


Muhaji amesema mkutano umejikita katika maeneo matatu ya msingi, ambayo ni sera na kanuni, upatikanaji wa mitaji na fedha, pamoja na upatikanaji wa masoko. Ameeleza kuwa majadiliano na Serikali yamefungua nafasi ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili wajasiriamali.


Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Tanzania Startup Association, Paul Makanza, amesisitiza umuhimu wa kuwaunganisha wajasiriamali na wawekezaji ili mawazo ya kibunifu yapate mitaji na nafasi ya kukua kibiashara.


Makanza amependekeza kuanzishwa kwa maeneo maalumu ya ubunifu yatakayowawezesha wajasiriamali kukutana, kufanya kazi na kuwasilisha mawazo yao kwa wawekezaji. Maeneo hayo yanaweza kushirikisha taasisi za kifedha na kampuni za mawasiliano ili kurahisisha upatikanaji wa huduma muhimu, ikiwamo intaneti.


Amesema soko la huduma za kidijitali barani Afrika lina fursa kubwa kutokana na matumizi ya simu na uwezekano wa teknolojia kutumika katika sekta mbalimbali, zikiwamo biashara, usafiri na nishati.


Wadau hao wameeleza kuwa ushirikiano kati ya Serikali, taasisi za kifedha, kampuni za mawasiliano na startups ni muhimu katika kuboresha mazingira ya biashara, kuvutia mitaji na kuhakikisha mawazo ya vijana yanageuka kuwa shughuli za kiuchumi zinazoweza kukua na kutoa fursa kwa wengine.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *