Na Jerome Mlaki wa Dar.
DAR ES SALAAM.
Imeelezwa kuwa uamuzi wa kuruhusu mabasi ya masafa marefu kufanya safari kwa saa 24 umeelezwa kuwa miongoni mwa mageuzi makubwa yaliyofanyika katika kuboresha huduma za usafiri wa barabara nchini.
Katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), iliruhusu mabasi yaliyokidhi masharti kusafiri usiku na mchana.
Hatua hiyo imeongeza muda wa huduma kwa waendeshaji wa mabasi na kuwapa abiria fursa zaidi za kuchagua muda wa kusafiri.
Hayo yameelezwa leo Septemba 24,2027 jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Dk. Habibu Suluo,wakati akizungumza na Wahariri na Waandishi wa habari katika Mkutano uliyoandaliwa na ofisi ya Msajiri wa Hazina,
nakubainisha kuwa uamuzi huo uliwezekana kutokana na kuimarika kwa usalama, miundombinu ya barabara, mifumo ya mawasiliano pamoja na uwezo wa LATRA kufuatilia mabasi kupitia Mfumo wa Ufuatiliaji wa Magari (VTS).
Amesema tathmini zinaonesha kuwa huduma ya safari za usiku imechangia kupunguza ajali na msongamano katika vituo vya mabasi, huku pia ikipunguza ushindani miongoni mwa baadhi ya madereva wa kuendesha kwa mwendokasi hatarishi ili kuwahi kufika wanakoelekea.
Aidha,amesema abiria wengi wamekuwa wakipendelea kusafiri usiku kwa sababu huduma hiyo imepunguza au kuondoa hitaji la kugharamia malazi, hususan wafanyabiashara wanaosafiri kati ya mikoa mbalimbali.
Halikadhalika Dk. Suluo,ameongeza kuwa kuanza kwa safari za usiku kumeongeza fursa za biashara na uwekezaji katika sekta ya usafirishaji,pamoja na kuongeza ufanisi wa matumizi ya miundombinu ya barabara na kudhibiti uchovu wa madereva





0 maoni:
Chapisha Maoni