Na. Jerome Mlaki wa Dar.
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza kuwa msimu wa Ligi ya NBC Championship kwa mwaka 2026/2027 unatarajiwa kuanza rasmi Oktoba 29, 2026 na kukamilika Mei 27, 2027.
Hayo yamesemwa Agosti 28, 2026, jijini Dar es Salaam na Afisa Mtendaji Mkuu wa TPLB, Cornel Barnabas, wakati akizungumza kuhusu maandalizi ya msimu mpya wa ligi hiyo.
Barnabas amesema ratiba ya msimu huo imeandaliwa kwa kutumia mfumo wa kidijitali, hatua inayolenga kuwezesha upangaji wa michezo kuwa wenye ufanisi na kuzingatia mahitaji ya mashindano.
“Ratiba imeandaliwa kidijitali, hivyo nazitakia maandalizi mema timu zote zitakazoshiriki katika mtanange huo,” amesema Barnabas.
Kutangazwa kwa tarehe ya kuanza kwa msimu huo kunazipa klabu zinazoshiriki NBC Premier League nafasi ya kuendelea na maandalizi kuelekea msimu mpya, huku mashabiki wa soka nchini wakisubiri kwa hamu kuanza kwa ushindani mwingine wa kuwania ubingwa.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kuhusu ratiba ya msimu wa 2026/2027, NBC Premier League inaendelea kuwa miongoni mwa mashindano yanayofuatiliwa kwa karibu katika soka la Tanzania.
Kwa upande wake,Afisa Habari wa TPLB, Yahaya Abusheh, amesema msimu huo utashirikisha jumla ya timu 16, ambazo zitagawanywa katika makundi mawili.
Amesema kundi A litakuwa na timu nane, huku kundi B likiwa na timu nane





0 maoni:
Chapisha Maoni