WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumatatu, 6 Novemba 2023

 06:00      No comments

 Torintohot

Jerome Mlaki wa Dar.



SAMAKI aina ya Dagaa mchele na Saladini wameadimika katika mwambao wa Bahari ya Hindi na kusababisha upandaji wa bei wa kitoweo hicho mkoani Dar es Salaam.



Torintohot media Blog. lilifika katika soko hilo Novemba 4, 2023 nakushuhudia umati mkubwa wa wafanyabiashara wa Samaki kutoka maeneo mbalimbali ya viunga vya Dar es Salaam wakisubiri wavuvi na wafanyabiashara wa jumla kufika katika soko la Kimataifa la Samaki Feri kwa ajili ya ununuzi wa Samaki.


Kuanzia alfajiri hakukuwa na mfanyabiashara wala mtumbwi wowote uliofikisha Samaki aina ya dagaa mchele wala saladini hadi ilipofika majira ya saa 4;30 asubuhi ndipo mfanyabiashara mmoja jina lake halikuweza kufahamika kwa haraka alifika katika soko hilo akiwa na vikapu vitano vya dagaa ambapo wafanyabiashara wa rejareja walimvamia kwa ajili yakupatiwa huduma hiyo.


Torintohot media Blog baada ya kushuhudia hali hiyo lilifanya mahojiano na Ofisa Uvuvi wa soko hilo Abeid Shamte ili kufahamu uhaba huo ambao siyo kawaida yake kwa majira ya Novemba alisema kuna uhaba wa Samaki tofauti na ilivyotarajiwa.



“Kama Mwandishi unakumbuka ulivyokuja Septemba 2023 nilikueleza sababu za kitaalamu za ukosekanaji wa Samaki nikikuahidi endapo hakutakuwa na mabadiliko ya tabia nchi huenda Samaki wangeliongezeka n ani kweli katikati mwa Oktoba Samaki walianza kupatikana kwa wingi lakini mwanzoni mwa Novemba hali imebadilika zaidi na kuwa ya hovyo juu ya upatikanaji wa Samaki” alisema Shamte


Aidha Shamte anatabaisha wazi kwamba sababu ni zilezile za mabadiliko ya tabia nchi, lakini uadimikaji wa awali na wasasa una tofauti yake, kwasababu mwezi Mei hadi Septemba ni msimu wa baridi kwa ukanda wa mwambao wa Pwani na hakuna mvua kali na ngurumo lakini safari hii kuna mvua kubwa zilizoanza Nomba ,2023.



“Samaki ana tabia moja Bahari inapochafuka hususani mvua zinazo sababisha mito kufurika na kuelekea Baharini kunakosekana kwa utulivu na hivyo Samaki hutafuta maficho zaidi kwasababu maji yaingiayo Baharini huja na takataka, udongo na kila aina ya uchafu hivyo husombwa na maji kuelekea umbali mrefu ambapo hata wavuvi wakati mwingine hawezi kufika” alisema



Torintohot media Blog lilizungumza na wafanyabiashara sokoni hapo ili kubaini bei ya Samaki kwa ndoo ya lita 20, ambapo walisema bei ya dagaa mchele imetoka Sh 30,000 hadi Sh 100,000 baada ya wiki mbili zilizopita na Ndoo ya saladini imetoka kutoka Sh 40,000 hadi Sh 100,000.




Kutokana hali hiyo Samaki kwa upande wa rejareja huko mitaani bei yake haijapanda ispokuwa vipo vya ujazo vimekuwa finyu mno kwa maana ya ukadiriaji wa mafungu bado fungu ni Sh 1000 lakini halina ukubwa kama ule wa kipindi Samaki wanapopatikana kwa wingi.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *