WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Alhamisi, 26 Oktoba 2023

 06:14      No comments

 

Na torintohot media Blog.

Na Jerome Mlaki wa Dar.

Tell. 0789106710


Dk. Biteko Atembelea Banda la Barrick Mkutano wa Jukwaa la Kimataifa la Uwekezaji katika Sekta ya Madini




Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk.Doto Biteko, akipata maelezo ya utendaji wa kampuni ya Barrick kutoka kwa Makamu wa Rais wa wa Utafiti wa Madini wa Barrick kanda ya Afrika na Mashariki ya Kati , Nathan Komarnisky, wakati alipotembelea banda la Barrick kwenye mkutano wa Tanzania Mining Investment Forum Kulia ni Waziri wa Madini Anthony Mavunde.



Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko akisalimiana na Makamu wa Rais wa Utafiti wa madini wa Barrick kanda ya Afrika na Mashariki ya Kati, Nathan Komarnisky, wakati alipotembelea banda la Barrick mkutano wa Jukwaa la kimataifa katika sekta ya madini (Kulia) ni Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde


Waziri wa Madini,Antony Mavunde, akisalimiana na Makamu wa Rais wa Utafiti wa Madini wa Barrick kanda ya Afrika na Mashariki ya Kati, Nathan Komarnisky, wakati alipotembelea banda la Barrick lililopo kwenye mkutano wa Jukwaa la kimataifa katika sekta ya madini


Meneja wa Barrick nchini, Melkiory Ngido, akieleza mafanikio yaliyopatikana kutokana na ubia wa Barrick na Twiga katika kukuza uchumi wa nchi na kuboresha maisha ya wananchi kwa wajumbe wa mkutano wa kimataifa wa sekta ya madini (Tanzania Mining Investment Forum)



Washiriki mbalimbali wamekuwa wakitembelea banda la maonesho la Banda la Bariki.


***


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko, ametembelea banda la maonesho la Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Barrick inayoendesha shughuli zake nchini kwa Ubia na Serikali kupitia Kampuni ya Twiga katika mkutano wa Jukwaa la Kimataifa katika Sekta ya Madini (Tanzania Mining Investment Forum) unaoendelea jijini Dar es Salaam na kupata maelezo ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni kupitia migodi yake iliyopo nchini ya Bulyanhulu, North Mara na Buzwagi, sambamba na mafanikio yaliyopatikana tangu Barrick ianze kuendesha migodi nchini.


Dk. Doto Biteko alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano huo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.Samia Suluhu Hassan.


Meneja Mkuu wa Barrick nchini, Melkiory Ngido, alitoa wasilisho katika mkutano huo wa kimataifa na kubainisha mafanikio yaliyopatikana kutokana na ubia wa Barrick na Twiga nchini katika uchimbaji wa madini ambao umefanikisha kuleta mapinduzi mbalimbali yenye tija ikiwemo kutoa mchango katika pato la Taifa, kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania, kutekeleza miradi ya huduma za kijamii kupitia sera ya CSR, kuboresha sekta ya elimu sambamba na kuinua maisha ya wazabuni wa kitanzania.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *