WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Ijumaa, 1 Juni 2018

 07:09      No comments

Torinto Hot Blog.
Na.. Jerome Mlaki Dar.

28

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa  Kongamano la Mabadiliko ya Tabia Nchi, Mazingira na Uchumi wa Taifa  lililoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania na kufanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
17
Balozi wa Sweden nchini Mhe. Katarina Rangnitt akihutubia wakati wa ufunguzi wa  Kongamano la Mabadiliko ya Tabia Nchi, Mazingira na Uchumi wa Taifa  lililoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania na kufanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
25
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba  akihutubia wakati wa ufunguzi wa  Kongamano la Mabadiliko ya Tabia Nchi, Mazingira na Uchumi wa Taifa  lililoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania na kufanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amesema kuwa ongezeko la watu katika miji mikubwa kuna changia sana katika uharibifu wa mazingira na matumizi makubwa ya mkaa.
Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Mabadiliko ya Tabia Nchi, Mazingira na Uchumi wa Taifa lililofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais amesema “Mkaa ni Ghali Tutumie Nishati Mbadala”, kwani kiwango cha miti inayokatwa kwa ajili ya kutengeneza mkaa ni kikubwa na kinatisha.
“ Dar es Salaam peke yake inakadiriwa kutumia kati ya magunia kati ya 200,000 mpaka 300,000 yenye uzito wa kilo 50 kila moja ya mkaa kwa mwezi na inategemewa itaongezeka zaidi kutokana na kasi ya ongezeko la watu hasa kwenye miji ” alisema Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais amewata Watanzania, Makampuni pamoja na Taasisi mbalimbali kuungana na Serikali kubadilisha jamii yetu kuanza kutumia nishati ya majani kwa namna ya mkaa na kuni kama vyanzo mbadala vya nishati endelevu.
Makamu wa Rais amesema kuwa kilele cha Siku ya Mazingira ni tarehe 5 Juni, 2018 ambapo dhima ya Kimataifa ni Kupiga Uchafuzi wa Mazingira unaotokana na Plastiki (Beat Plastic Pollution) lakini Tanzania imelekeza nguvu zake katika kuadhimisha siku hiyo kwa kuwataka Wananchi wake wabadilike badala ya kutumia mkaa ambao unasababisha ukataji mkubwa wa miti ni vyema kuanza kutumia nishati mbadala.
Mapema; Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mheshimiwa January Makamba alisema kutokana na uhitaji na umuhimu wa kutunza mazingira Serikali, Wadau wa Maendeleo, Taasisi mbali mbali, Sekta Binafsi na Watungaji wa Sera kutafakari kwa pamoja na kuja na majawabu yatakayosaidia katika utunzaji wa mazingira na kuilinda miti.

Wakati huo huo;  Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mhe. Katarina Rangnitt amesema tangu mwaka 1972 changamoto za uharibifu wa mazingira hazikuwa za Kikanda tu bali ni kwa dunia nzima hivyo hili jambo linahitaji ushiriki wa Dunia nzima katika kupambana na uharibifu wa mazingira.ngamano la Mabadiliko ya Tabia ya nchi, Mazingira na Uchumi wa Taifa

 TAGS
28
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa  Kongamano la Mabadiliko ya Tabia Nchi, Mazingira na Uchumi wa Taifa  lililoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania na kufanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
17
Balozi wa Sweden nchini Mhe. Katarina Rangnitt akihutubia wakati wa ufunguzi wa  Kongamano la Mabadiliko ya Tabia Nchi, Mazingira na Uchumi wa Taifa  lililoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania na kufanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
25
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba  akihutubia wakati wa ufunguzi wa  Kongamano la Mabadiliko ya Tabia Nchi, Mazingira na Uchumi wa Taifa  lililoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania na kufanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amesema kuwa ongezeko la watu katika miji mikubwa kuna changia sana katika uharibifu wa mazingira na matumizi makubwa ya mkaa.
Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Mabadiliko ya Tabia Nchi, Mazingira na Uchumi wa Taifa lililofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais amesema “Mkaa ni Ghali Tutumie Nishati Mbadala”, kwani kiwango cha miti inayokatwa kwa ajili ya kutengeneza mkaa ni kikubwa na kinatisha.
“ Dar es Salaam peke yake inakadiriwa kutumia kati ya magunia kati ya 200,000 mpaka 300,000 yenye uzito wa kilo 50 kila moja ya mkaa kwa mwezi na inategemewa itaongezeka zaidi kutokana na kasi ya ongezeko la watu hasa kwenye miji ” alisema Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais amewata Watanzania, Makampuni pamoja na Taasisi mbalimbali kuungana na Serikali kubadilisha jamii yetu kuanza kutumia nishati ya majani kwa namna ya mkaa na kuni kama vyanzo mbadala vya nishati endelevu.
Makamu wa Rais amesema kuwa kilele cha Siku ya Mazingira ni tarehe 5 Juni, 2018 ambapo dhima ya Kimataifa ni Kupiga Uchafuzi wa Mazingira unaotokana na Plastiki (Beat Plastic Pollution) lakini Tanzania imelekeza nguvu zake katika kuadhimisha siku hiyo kwa kuwataka Wananchi wake wabadilike badala ya kutumia mkaa ambao unasababisha ukataji mkubwa wa miti ni vyema kuanza kutumia nishati mbadala.
Mapema; Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mheshimiwa January Makamba alisema kutokana na uhitaji na umuhimu wa kutunza mazingira Serikali, Wadau wa Maendeleo, Taasisi mbali mbali, Sekta Binafsi na Watungaji wa Sera kutafakari kwa pamoja na kuja na majawabu yatakayosaidia katika utunzaji wa mazingira na kuilinda miti.
Wakati huo huo;  Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mhe. Katarina Rangnitt amesema tangu mwaka 1972 changamoto za uharibifu wa mazingira hazikuwa za Kikanda tu bali ni kwa dunia nzima hivyo hili jambo linahitaji ushiriki wa Dunia nzima katika kupambana na uharibifu wa mazingira.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management

CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio

Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *