WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumanne, 8 Mei 2018

 07:52      No comments


 TAGS


Torinto Hot Blog.

Na. Jerome Mlaki. Dar

Waziri wa nchi ofisi ya Rais serikali za mitaa Tamisemi Mhe. Suleiman Jafo amtoa siku 45, kwa mamlaka husika katika soko la Ferry lililopo katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam kufanya Ukarabati wa miundo mbinu ya soko hilo ambayo imeharibika na kusababisha mazingira magumu ya kazi kwa wafanyabiashara wa eneo hilo.

Waziri Jafo ameyasema hayo leo katika ziara aliyoifanya katika soko hilo ambapo amekagua miundo mbinu mbalimbali ikiwepo barabara, ya soko hilo,meza choo pamoja na maji ambapo amesema wafanyabiashara hao wanalipa kodi hivyo ni haki yao kuwepo kwa miundo mbinu rafiki na salama kwao.

"Nitakuja hapa baada ya siku 45, kuona mazingira yamerwkebishwa na nitoe maelekezo kwa Injinia ahakikishe barabara hii imetengenezwa na tarehe 23, mwezi Julai nitakuja hapa kuangalia utekelezaji ukarabati wa mazingira haya kwani hili ni soko kubwa ambalo linakuza uchumi wao na wa nchi kwa ujumla"Amesema Jafo.

Aidha amesema anataka wakina  Mamantilie waliokuwa wakifanya biashara katika eneo hilo na kutolewa warudishwe na kuwataka akina Mamantilie hao kufuata sheria na kuwa mlinzi kwa kila mmoja kuhakikisha wanaofanya biashara za madawa ya kulevya wanabainishwa.

" Nataka wakina mama waliokuwa wanafanyabiashara ya chakula hapa Sokoni warudishwe na kuendelea na kazi zao ili kuwarahisishia wafanyabiashara kupata chakula kwa urahisi na kuwataka Mamantilie hao kuhakikisha kila mmoja anakuwa mlinzi wa mwenzake ili kubaini wanaopita na kutumia madawa ya kulevya"Amesema

Waziri Jafo amesema kuwa ameuzunishwa na uongozi unavyofanya kazi katika eneo hilo kwani wananchi wanapata shida kutokana na miundo mbinu mibovu.

Pia amemtaka Meneja wa soko kuhakikisha wanatenga sehemu za wakina Mama Ntilie ili waendelee kufanya biashara kutokana na kutolewa maeneo hayo kwa tuhuma za kujihusisha na madawa ya Kulevya.

"Meneja wa Soko hakikisha mnatenga sehemu maalumu ya  kina Mamantilie ili waweze kuendeleza biashara yao na wanaofanya shughuli zao hapa waweze kuwa na uhakika wa kupata chakula sehemu salaam na rahisi kwao"Amesema Waziri Jafo.

 Pia ameutaka uongozi kuhakikisha wanatatua changamoto zilizopo katika soko hilo kwani ni sehemu kubwa ambayo wananchi wanaofanya biashara zao na kujipatia kipato cha kuendesha maisha yao,pamoja na kuinua uchumi wa nchi na si kusubiri waziri afike kutoa maelekezo.

Kwa Upande wake Meneja wa Soko la Ferry Mkuu .B. Hanje amesema kuna Jengo ambalo lipo katika soko hilo na kwamba linadaiwa kuwa ni la halmashauri ya Manispaa ya Ilala ambapo hawakusanyi Kodi kutoka katika jengo hilo hivyo wanashindwa kulikarabati kutokana na kuwa liko chini ya manispaa.

Amesema watahakikisha yote aliyoyasema Mhe. Waziri yanafanyiwa kazi kikamilifu na kuondoa kero na changamoto zilizopo.

Nao wafanyabiashara wa soko hilo wamekiri kuwepo kwa changamoto hizo ,na wamemshukuru Mhe. Waziri kwa kufika na kuwasaidia ili changamoto hizo ziweze kutatuliwa na kuweza kufanya kazi Katika mazingira rafiki na salaama ili kukuza uchumi wao binafsi na taifa kwa ujumla.Facebook

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *