WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Alhamisi, 2 Novemba 2017

 00:13      No comments
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akipata maelezo kuhusu aina ya vitabu vinavyotumika kufundishia Elimu ya Watu Wazima kutoka kwa Mratibu wa Progaramu ya Elimu Changamano nje ya mfumo rasmi Dkt. Sempeho Siafu kutoka katika Taasisi ya Elimu


Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiangalia baadhi ya mitambo inayotumika kuandaa vipindi vya elimu kwa umma katika studio zilizoko  Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.

Naibu Mkurugenzi Utafiti na Ushauri Dkt. Kassimu Nihuka akifafanulia Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiangalia matumizi ya mashine za uchapaji zilizopo katika karakana ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.


Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Ole Nasha ameitaka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kuendelea kutekeleza majukumu yake ya kimuundo badala ya kufikiria kufanya miradi ambayo imekuwa ikiwaondoa kwenye mwelekeo wa malengo ya uanzishwaji wa Taasisi hiyo.

Naibu Waziri Ole Nasha ametoa wito huo leo jijini Dar es Salaam alipotembelea Taasisi hiyo  ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kuzitambua taasisi zilizo chini ya wizara pamoja na utendaji wa majukumu yake.

Akiwa katika Taasi hiyo amesema nchi bado inaihitaji Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima pamoja na aina ya elimu ambayo inatolewa na taasisi hiyo, hivyo ameitaka taasisi hiyo  kutekeleza majukumu yake iendane na hali halisi ya mazingira ya elimu.

Ole Nasha mesema
 ukiangalia utekelezaji wa miradi  hiyo inabaki kuitwa elimu ya watu wazima lakini namna inavyoendeshwa haziakisi uhalisia wake na badala yake zinabaki kuwa kama mifumo mingine ya utoaji wa elimu ya mfumo rasmi.

Naibu Waziri Ole Nasha akiwa katika taasisi hiyo amepata fursa ya kutembelea chumba cha Uchapaji vitabu  majarida, Karakana, Maktaba na idara ya Elimu ya masafa na Studio za kuandaa vipindi vya kuelimisha umma vya Elimu ya Watu Wazima.

Aidha, Naibu Waziri ametembelea Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Elimu, Habari, utamaduni  ya UNESCO na kuwataka kuitisha kikao cha wadau wanaohusika na Tume hiyo ili kuzungumzia changamoto za kimfumo na muundo zinazoikabili taasisi hiyo.

Imeandaliwa na kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizar ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

31/10/2017

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *