WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Ijumaa, 27 Oktoba 2017

 04:58      No comments


Torinto Hot Blog
Wanafunzi kutoka chuo cha Bahari nchini (DMI) wamefanya zoezi la kufundisha abiria wanaotumia
kivuko cha Magogoni Kigamboni jinsi ya kutumia vifaa vya kujiokolea vilivyomo katika vivuko hivyo pindi inapotokea dharura ya ajali kwenye maji.

Zoezi hilo lililoratibiwa na chuo cha Bahari kwa kushirikiana na kitengo cha Habari na Mawasiliano
(TEMESA) limefanyika kivukoni hapo mapema asubuhi likiongozwa na Nahodha Nyamurasa Matage
kutoka chuo hicho. Zoezi hilo lilihusisha wanafunzi wa kozi ya PST na lilikua na nia ya kuwaonyesha
watumiaji wa kivuko hicho namna ya kujiokoa na pia kujifunza kuwa na utulivu pindi inapotokea dharura ya ajali, moto au kuzimika kwa kivuko.

Akizungumza katika tukio hilo Nahodha Nyamurasa aliwataka watumiaji wa kivuko hicho kuhakikisha
wanafuatilia kwa makini zoezi hilo kwani dharura ya ajali inaweza kutokea wakati wowote na mahala
popote hivyo abiria wanatakiwa kuwa watulivu pindi inapotokea. Alisema mafunzo hayo yalikua ni
sehemu ya masomo yao ya darasani lakini pia elimu tosha kwa watumiaji wa vivuko.

Naye Mkuu wa kivuko Magogoni Kigamboni Mhandisi Lukombe King’ombe akizungumza wakati wa zoezi hilo aliwataka wanafunzi hao kulichukulia kwa umakini zoezi hilo kwani pindi wanapomaliza mafunzo yao wanatumiwa katika vivuko vya TEMESA katika shughuli za uokoaji wa abiria na mali zao na pia kutoa maelekezo ya usalama kwa abiria wa vivuko hivyo.

“Hili ni zoezi muhimu kwa abiria wetu kulipata na kujifunza namna ya kutumia vifaa vya kujiokolea ambavyo vinakuwepo muda wote katika vivuko vyetu,” alisema King’ombe.

Dhumuni kubwa la zoezi hilo lilikua ni kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa Chuo hicho na pia kutoa
mafunzo kwa abiria wanaotumia kivuko. Zoezi hilo linategemewa kuendelea wiki ijayo katika kivuko
hicho.


0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *