Kamanda wa polisi kanda maalum dar es salaam, akizungumza na waandishi wa habari leo jijini dar es salaam.
Shekhe Ponda Issa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari,Siku ya Jana na kufanikiwa kukimbia polisi baada ya kufahamu kuwa anatafutwa.
Na Michael utouh
Shekhe Ponda Issa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari,Siku ya Jana na kufanikiwa kukimbia polisi baada ya kufahamu kuwa anatafutwa.
Na Michael utouh
Kamanda Polisi wa kanda maalumu Dar es salaam Lazaro Mambo Sasa SACP ametoa taarifa mbele ya vyombo vya Habari kuwa jeshi la polisi kanda maalumu linamtafuta katibu wa jumuiya ya taasisi za kiislamu Tanzania Shekhe Ponda Issa Ponda kwa tuhuma za kutoa lugha zenye kuashiria uchochezi pamoja na kuikashifu serikali.
Akizungumzia sakata hilo ambalo limekuwa ni gumzo kubwa Mara baada ya tukio la Jana tarehe 11.10.2017 lililotokea la Shekhe huyo kuita vyombo vya Habari na kuzungumza nao na Mara baada ya kugundua kuwa anatafutwa ndipo alipoamuwa kuwatoroka polisi waliokuwa wakimtafuta.
Hata hivyo Kamanda Mambosasa ameongeza kwa kusema wao wamejipanga vilivyo hivyo Shekhe Ponda asijifanye kuwa anajaribu kufanya mchezo wa kuwatoroka polisi hivyo akampa siku Tatu tuu kutoka Leo hii ajisalimishe mwenyewe kwa ofisi za ZTO(ofisi za upelelezi wa makosa ya jinsi) na baada ya hapo kama hatojisalimisha wao wataanza kumtafuta mwenyewe.
"Ponda kwanza ana makosa mengi ya kijinai pia hata matamshi yake Mara nyingi yamekuwa ni ya kiuchochezi au kuikejeli serikali hivyo kupitia kwenu wanahabari nakuomba huyo Shekhe Ponda ajisalimishe mwenyewe kwa ajili ya mahojiano na kama tukiridhika na mahojiano yake basi atakuwa huru lakini ikiwa tofaut lazima tutampeleka mahakamani" Amesema Kamanda Mambo sasa.
Mara kwa Mara Shekhe huyo amekuwa akiwa kwenye wakati mgumu na kujikuta akiishi Maisha ya wasiwasi Maisha ya kuwindwa hasa baada ya matamshi yake ambayo amekuwa akiyatoa Mara kwa Mara juu ya serikali na dola kiujumla.
Hata hivyo polisi walishindwa kumkamata kwa wakati hapo Jana alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari katika moja ya hoteli iyopo kariakoo na kuwatoroka askari hao pale alipogundua
0 maoni:
Chapisha Maoni