WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumatatu, 17 Julai 2017

 06:57      No comments
Haya ndiyo yaliyojiri kwenye soko la hisa wiki iliyoisha Ijumaa tarehe 14 Julai 2017.
Mauzo ya Hisa (Turnover/ Liquidity)
Thamani ya mauzo ya  hisa kwa wiki hii imepungua  kwa 36% kutoka Shilingi bilioni 6 wiki iliyopita hadi Shilingi bilioni 3.9 wiki hii iliyoishia tarehe 14 Julai 2017.
Hata hivyo idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imepanda kwa 26% kutoka hisa 13.6 wiki iliyoisha tarehe 6 Juni 2017, hadi hisa milioni 17 kwa wiki iliyoishia 14 Julai 2017.
Kampuni zilizoongoza katika mauzo ya hisa ni kama ifuatavyo:
CRDB     …………………………………………..……89%
TBL      ……..…….………………..…………..………8%
DSE       …….....……..……….…………....………… 0.9%
Ukubwa Mtaji (Market Capitalization)
Ukubwa wa mtaji wa kampuni zilizoorodheshwa katika soko umepanda kwa Shilingi Bilioni 516 kutoka Shilingi Trilioni 18.7 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 19.2 wiki iliyoishia tarehe 14 Julai 2017. Hii ni kutokana na kupanda kwa bei za hisa za USL (34%), ACA (9%) na JHL (5%).
Ukubwa wa mtaji wa kampuni za ndani umepanda kwa Shilingi Bilioni 13.5 kutoka Shilingi Trilioni 7.70 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 7.72 wiki hii. Hii ni kutokana na kupanda kwa bei ya hisa za CRDB (2.5%).
Hati Fungani (Bonds)
Tofauti na ilivyokuwa kwenye hisa, mauzo ya hati fungani katika wiki iliyoishia tarehe 14 Julai 2017 yamepanda kutoka Shilingi bilioni 12.25 wiki iliyopita hadi Shilingi Bilioni 44.3
Mauzo haya yalitokana na hatifungani kumi na saba (17) za serikali na za Makampuni binafsi                        (Corporate Bonds) zenye jumla ya thamani ya Shilingi bilioni 51 kwa jumla ya gharama ya Shilingi Bilioni 44.3.

Viashiria (Indices)
Kiashiria cha kampuni zilizoorodheshwa katika soko yaani DSEI kimepanda kwa pointi 59 kutoka pointi 2,151 hadi pointi 2,211 kutokana na kuongezeka kwa bei za hisa za kampuni mbali mbali zilizopo sokoni.
Kufuatia kupanda kwa bei za hisa, kishiria cha kampuni za ndani yaani TSI kimepanda kwa pointi 6 kutoka pointi 3,666 wiki iliyopita hadi pointi 3673 wiki hii.
Kiashiria cha sekta ya viwanda (IA) imebaki kama awali kwenye wastani wa TZS 4809
Kiasharia cha huduma za kibenki na kifedha (BI) wiki hii kimepanda kwa pointi 17 kutoka pointi 2,598 hadi pointi 2,616 kutokana na ongezeko la bei ya hisa za CRDB (2.5%)
Kiashiria cha Sekta ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii imebaki kwenye wastani wa 2,467 kama awali.

Shindano la Wanafunzi la Uwekezaji
Shindano la DSE SCHOLAR INVESTMENT CHALLENGE 2017 lilifika mwisho tarehe 30 Juni 2017. Zaidi ya wanafunzi wa vyuo na secondary 12,000 walishiriki katika shindano la mwaka huu, ikiwa ni Zaidi ya mara 3 ya mwaka uliopita, 2016.
Matokea ya washindi wa shindano hili yatatangazwa tarehe 18 July 2017 baada ya kufanyika tukio la mwisho la kuhusisha wanafunzi 10 bora kushiriki katika kipindi cha maswali na majibu na washindi  watatu (3) kuamuliwa na jopo ya majaji wa shindano hili.




0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *