'Siku ya jua' mjini Pyongyang iliadhimishwa kwa maonyesho ya makombora, mwendo bila kukunja magoti na mapambo ya nguo (pom-poms)
- Korea Kaskazini imeandaa gwaride kubwa na la kusisimua katika mji mkuu Pyongyang kuadhimisha miaka 105 tangu kuzaliwa kwa kiongozi mwanzilishi wa taifa hilo, Kim Il-sung.
- Maadhimisho hayo yanajulikana kama 'Day of the Sun' ama siku ya jua, kwani Kim Il-sung mara nyingi huwa anatambulishwa kwa ishara jua.
- Maadhimisho hayo yalionekana kama maonyesho ya nguvu za kijeshi wakati kumekuwa na uhusiano baridi baina ya Marekani na Korea Kaskazini.
- Mwandishi wa BBC aliyehudhuria maadhimisho hayo anasema kwamba alihisi ardhi ikitetemeka wakati wanajeshi walipokuwa wakipita pamoja na makombora.
- Wanajeshi wanawake wakitembea bila kukunja magoti katika onyesho la kusisimua.
- Bendera ya Korea Kaskazini ilipeperushwa kwa nguvu.
- Kundi la wanaume wakiwa wamebeba mapambo yanayowekwa kwenye nguo ama kofia (pom-poms)
- Ndege angani zimeunda umbo la takwimu 105.
- Kiongozi wa Korea Kusini Kim Jong-un, mjukuu wa rais mwanzilishi wa taifa hilo, awapungia mkono watu waliohudhuria maadhimisho hayo.
- Mwanajeshi apiga picha za maadhimisho hayo.
0 maoni:
Chapisha Maoni