WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Ijumaa, 17 Machi 2017

 03:14      No comments

 TAGS
Baada ya hivi karibuni msanii wa hip hop, Nay wa Mitego kutangaza kuwa atafungua kanisa lake ambalo litakuwa si la biashara bali ni la kumuabudu Mungu aliye hai, Mchungaji maarufu nchini, , Lusekelo Anthony aka Mzee wa Upako amemuonya kutomchezea Mungu. 

Mzee wa upako ameyasema hayo alipotafutwa na E-News ya EATV baada ya kuulizwa maswali juu ya kauli hiyo.

“Kama unakuja kanisani kwa maana kuna biashara, nakupa miaka hii mitatu sio utatembelea ndala utatembelea kucha, ni mtoto mdogo sana hana akili. 
"Mungu hataniwi, anafanya kufuru, kama ana mama yake amemzaa amuonye. Mimi biblia nimesoma na hizo lugha zake nyepesi zitamtokea puani, asithubutu kufanya kanisa kama biashara. 
"Baada ya miaka hii mitatu atajua kwamba kuongoza watu sio kama kuongoza ngo’mbe hakuna jambo gumu kama kuongoza watu wenye akili kama wewe wenye ufahamu kama wewe, wapo watu wengi walianzisha makanisa kwanini walifunga, ujinga hujui ni ujinga ni utoto,” alisema Mzee wa Upako.

Nay amedai kuwa kanisa lake litajengwa Mbezi ya Kimara jijini Dar es Salaam.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *