WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumatano, 30 Novemba 2016

 04:46      No comments
shirika la maendeleo la petrol tanzania(TPDC) limekanusha tarifa zinazoenezwa kampuni ya dangote pamoja na washirika wake kupitia mitandao ya kijamii, pamoja na vyombo vya habari vikidai kuwa TPDC imeshindwa kukiuzia gesi asilia kwa bei rahisi kiwanda cha saruji cha dangote kilichopo mkoani mtwara kwa kuwa moja ya sababu ya kusimamisha uzalishaji kiwanda hicho.

 Hivyo TPDC Imetoa taarifa kwamba inafanya jidihada mbalimbali, Kuhakikisha kampuni ya dangote inapata nishati hiyo muhimu kwa ajili ya kuzalisha saruji ikiwemo kufanya vikao mbalimbali vya pamoja na makubaliano yaliyofanyika kwa dangote kwa kuridhia nia yao kutumia gesi asilia kuzalisha umeme kwa ajili ya kiwanda cha saruji cha dangote kilichopo Mtwara.

Akizungumza na waandishi wa habari hii leo jijini Dar Es Salaam Kaimu Mkurugenzi wa shirika la maendeleo la petrol tanzania(TPDC) Eng. Kapuulya A. Musomba amesema TPDC hufuata sheria na kanuni na taratibu za kupanga bei za gesi asilia ambapo hupanga kulingana na aina ya mteja hivyo kwa wateja wamegawanyika kufuatia makundi tofauti kama vile wateja wa viwanda, majumbani, magari pamoja na wateja wa kuzalisha umeme hata hivyo bei elekezi inayopendekezwa na TPDC lazima iridhiwe na kupitishwa na EWURA ndipo ianze kutumika.

Dangote kama mtumiaji wa matumizi ya viwandani amekuwa na mazungumzo ya muda mrefu na TPDC kuhusu Gesi asilia. Kiwanda cha Dangote kimeomba kupewa gesi asilia kwa bei ambayo hapa kwetu tanzania ni kidogo kwani kiasi hicho cha bei ndicho kinacholipwa kununulia gesi gafi kutoka kisimani Kwenda kwa mtumiaji.

TPDC ni shirika la mafuta la taifa linalofanya kazi zake kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za inchi, na kuwajali wawekezaji akiwemo dangote ili wawekeze katika kukuza uchumi wa inchi hivyo si sahihi kusema TPDC imemkwamisha dangote katika uzalishaji wa saruji Mtwara.




0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *