Mwanariadha maarufu mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius amefutiwa mashitaka ya mauaji ya aliyekuwa mpenzi wake, Reeva Steenkamp.
Pistorius kupitia mlango wa choo alimlipiga mwanamitindo huyo risasi nne ziliztoa uhai wake lakini akasema alidhani wameingiliwa na mpenzi wake alikuwa chumbani kwao.
Lakini jaji Thokozile Masipa aliyekuwa anaendesha kesi hiyo kwenye mahakama ya Pretoria, Afrika Kusini amemfutia mashitaka ya mauaji kwa madai upande wa ushahidi haukutoa vilelezo vilivyojitosheleza.
Akisoma hukumu yenye kurasa 3,000 Jaji Masipa alisemamwanariadha huyo angeweza kupatikana na hatia kama ushahidi ungejitosheleza.
Alisema kutokana na ushahidi wa kila upande inaonekana mwanariadha huyo hakukusudia kwa kuwa alijaribu kujilinda.
Hata hivyo bado Pistorius atalazimika kusubiri kipande kingine cha kesi hiyo kuhusiana na kifo hicho.
Hivyo kimsingi kuna kesi ambayo itaendelea kusikilizwa baada ya yeye kuonekana hana hatia ya mauaji.
0 maoni:
Chapisha Maoni