WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Ijumaa, 23 Oktoba 2026

 11:19      No comments




Na Jerome Mlaki wa Dar. 0789106710

Usajili wa vituo vya Kulea watoto mchana na Watoto Wachanga 

UTARATIBU WA USAJILI WA VITUO VYA KULELEA WATOTO WADOGO MCHANA NA WATOTO WADOGO

1.0 Utangulizi

  Vituo vya kulelea watoto wadogo mchana, ni moja ya huduma za malezi makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto zinazotolewa katika taasisi zinazoratibiwa na kusimamiwa na Wizara chini ya Idara ya Ustawi wa Jamii.

Huduma hizi zilianza kutolewa mwaka 1967 wakati wa Vijiji vya Ujamaa kwa lengo la kuwapatia wazazi nafasi ya kushiriki kwenye shughuli za uzalishaji mali. Mwaka 1981 ilitungwa Sheria ya vituo vya kulelea watoto wadogo mchana na mwaka 1982 zilitungwa kanuni kwa ajili ya utekelezaji wa sheria hiyo ambapo taasisi za serikali ,mashamba makubwa, pamoja na watu binafsi waliazisha huduma hizo ikiwemo; Magereza ,Shirika la reli,mashamba ya mikonge na chai,viwanda vya sukari n.k.

Mwaka 1985 kilianzishwa chuo cha ustawi wa Jamii Kisangara-Mwanga kwa ajili ya kuzalisha walezi wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana na baadae kupanua wigo kwa watu binafsi na mashirika ya dini kuanzisha vyuo vya malezi kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya walezi nchini . Mwaka 2009 ilitungwa Sheria ya Mtoto ambapo Sheria hii iliunganisha Sheria zote zinazohusu watoto ikiwemo sheria ya vituo vya kulelea watoto wadogo mchana.

Huduma hii imegawanyika katika maeneo makuu matatu:

Vituo vya kulelea watoto wachanga vinavyotoa huduma kwa watoto walio na umri kuanzia miezi 3 hadi miaka 2 (Crèches),
Vituo vya kulelea watoto wadogo mchana vinavyotoa huduma kwa watoto walio na umri wa miaka 2 hadi miaka minne (Day Care Centers)
Vituo vya kulelea watoto wadogo mchana vinavyomilikiwa na jamii kwa watoto wa umri wa miaka 2 hadi minne (Community Based Day Care Centers).
2.0 Madhumuni ya kuanzisha vituo hivi

Vituo hivi vimeanzishwa kwa madhumuni yafuatayo:

Kuwapa nafasi zaidi wazazi wa watoto ili waweze kufanya kazi zao za uzalishaji mali bila kuwa na hofu juu ya usalama wa watoto wao wakati wa mchana.
Kuwapatia watoto mazingira bora yanayowawezesha kukuza akili, mwili, lugha, hisia zao pamoja na kuwakuza kijamii na kiutamaduni.
Kuwapatia watoto malezi bora,
Kuwapa mwongozo na mwenendo bora wa maisha, utii, heshima na ushirikiano.
e)Kubaini na kuendeleza vipaji vya watoto na kuwaandaa kwa ajili ya kujiunga na shule za awali na hatimaye shule za msingi
f)Kufanya utambuzi wa mapema wa watoto wenye mahitaji maalumu/ ukuaji usio wa kawaida kwa ajili ya kuwapatia afua stahiki.
g) Kukuza ujifunzaji wa mapema na uhamasishaji wa kila mtoto na kukuza ujuzi wa kukabiliana na changamoto

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *