WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumamosi, 17 Desemba 2022

 08:35      No comments

 

Torinto hot media Blog. 23 hrs ago  



Shirika la Umeme nchini limesema limefanikiwa kupunguza makali ya upungufu wa umeme kutoka wastani wa kati ya megawati 200 hadi 250 wiki iliyopita hadi kufikia wastani wa kati ya megawati 100 hadi 150 wiki hii.


Akizungumza mapema leo Desemba 16 2022 Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Bwana Maharage Chande amesema shirika tayari wameshakamilisha matengenezo ya mtambo mmoja wa kituo cha Kinyerezi namba II na umeshaanza kuzalisha megawati 45 za umeme ambazo zinaingia kwenye Gridi ya Taifa kuanzia tarehe 24 Novemba 2022.


Alisema pia wamekamilisha matengenezo ya mitambo miwili iliyopo katika kituo cha Ubungo namba III na tayari imeshaanza kuzalisha kati ya megawati 35 na 40 za umeme ambazo zimnaingizwa katika Gridi ya Taifa.


"Katika kuhakikisha shirika linachukua hatua za kukabiliana na upungufu wa umeme tayari tumeshakamilisha matengenezo ya mtambo wa kituo cha Kidatu ambao umeshaanza kuzalisha megawati 50 za umeme kwenye Gridi ya Taifa kuanzia tarehe 30 Novemba 2022 hivyo kwa kiasi fulani kutapunguza makali ya mgao wa umeme”Alisema bw. Chande.


Bw. Chande alibainisha kuwa tayali shirika hilo limeshakamilisha ufungaji wa mitambo miwili iliyopo katika kituo cha Kinyerezi namba I ambacho kinazalisha megawati 90 za umeme ambazo zinaingia katika Gridi ya Taifa.


Amesema pamoja na mvua kuendelea kunyesha kwenye baadhi ya maeneo nchini, lakini bado hali ya kiwango cha maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme haijawa ya kuridhisha.


“Kwa mfano kituo cha New Pangani Falls (NPF) kwa sasa kinazalisha megawati 7 badala ya megawati 68, kituo cha Hale kinazalisha megawati 4 badala ya megawati 10.5, kituo cha Kidatu kinazalisha megawati 145 badala ya megawati 204 na bwawa la Nyumba ya Mungu linazalisha megawati 4 badala ya megawati 8. Hali hii inalifanya Shirika kuendelea kutegemea zaidi uzalishaji wa umeme kwa kutumia gesi asilia kuliko kwa kutumia maji” Alisema Bw. Chande.


Aidha Bw. Chande aliongeza kuwa Shirika litaendelea kutoa taarifa juu ya hali ya umeme sambamba na kutoa ratiba za upungufu wa umeme kupitia tovuti ya http://www.tanesco.co.tz, sambamba na kutuma ujumbe mfupi wa maneno (SMS) pamoja na katika magroup ya whatsapp ya wateja wake nchini kote.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *