WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumanne, 8 Mei 2018

 07:20      No comments


Maiko Torinto Dar
Mh. Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Vingunguti,  Omary Kumbilamoto amewashukuru Viongozi wa Manispaa ya  Ilala  na wananchi wa Wilaya hiyo kwa  ushirikiano wao walio onesha katika kisomo cha hitima ya Mama yake mzazi iliyofanyika  Kijijini  Kauzeni Wilayani Kisarawe.
 
Picha Zote Na. Torinto Hot Blog.

Kumbilamoto Ameyasema hayo leo Kijijini Kauzeni wakati wa Hitima ya Marehemu  Mama yake  na kuwataka  kuendelea na moyo huo wa kusaidia na kufarijiana katika wakati wa matatizo  bila kujali itikadi zao.

 "Napenda pia ni mshukuru Shekh mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Shekh Mussa Alhadi na pia nimtakie afya njema nimeambiwa anaumwa na ametuma  Mwakilishi wake , pia natoa shukrani zangu kwa mkuu wa wilaya ya Ilala Mhe.Sophia Mjema na uongozi wa Halimashauri ya Manispaa ya Ilala kwa ushirikiano wao Inshaallah Mwenyezi Mungu awazidishie "Amesema

Nao baadhi ya viongozi wa Dini na wananchi waliohudhuria hitima hiyo wamemzungumzia  Kumbilamoto la moto kuwa ni kiongozi wa tofauti anayejishusha bila kujali cheo na madaraka aliyo nayo na kuwa ni mfano wa kuigwa katika Jamii.

" Ni agharabu Sana kwa viongozi kuwa na moyo kama wa huyu Naibu Meya kwakweli mi na muombea  mwenyezi Mungu ili aweze kuambukiza na wengine  wawe na moyo kama yeye na washirikiane." Amesema mwananchi ambaye ameomba jina lake lihifadhiwe.


0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *