WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumanne, 10 Oktoba 2017

 03:48      No comments


Diterbitkan 

 TAGS
Ajiri namba moja barani Afrika Aliko Dangote ambaye pia ni mwekezaji mkubwa hapa nchini amemtahadhariha  Rais John Pombe Magufuli kuwa sera zake mpya zinawaogopesha wawekezaji.

Dangote ambaye amewekeza dola za kimarekani 650 kwenye uzalishaji wa saruji, amesema ni wakati umefika kwa raisi Magufuli kuzipitia upya sera zake ama akubali kuingia katika hatari ya kuwapoteza wawekezaji wote nchini .

Dangote ameyasema hayo katika mkutano wa FT Afrika unaofanyika London Uingereza na kuhudhuriwa na watu mashuhuri kutoka maeneo mbalimbali duniani.

Mwekezaji huyo ameeleza kuwa Uhusiano wake na Rais Magufuli ni mzuri lakini  akashauri Rais  azipitie  upya sera zake kama anataka kuwavutia waekezaji wengi zaidi.

“Uhusiano wangu na Rais Magufuli uko sawa lakini Tanzania lazima itazame upya sera zake kama inataka kuvutia wawekezaji,” alisema Dangote.

Dangote pamoja na watu wengine mashuhuri wakiwemo viongozi wa maeneo mbalimbali duniani wamehudhuria mkutano huo wa FT Africa wenye lengo la kuangazia changamoto zinazolikumba bara la Afrika na namna ya kuzitatua unaofanyika kila mwaka na mwaka huu umefanyika huko London, Uingereza kuanzia  Oktoba 8 hadi Oktoba 9.

Kauli mbiu ya mkutano huo ni ‘what is working in Africa’ ikiwa na maana ya ‘nini kinachofanya kazi katika Afrika’ ikiwa na dhumuni la kuangazia ni kwa namna gani bara hilo linaweza kunufaika kutokana na fursa, rasilimali na utajiri uliopo humo.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *