WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumanne, 23 Mei 2023

 13:49      No comments







NA Jerome Mlaki wa DAR.

WAZIRI wa Madini Dkt Dotto Biteko amezindua kongamano(Mkutano) la uwekezaji katika sekta ya madini utakaofanyika kuanzia tarehe 25-26 October 2023 nchini Tanzania, Tukio la uzinduzi umefanyika leo Jumanne 23,Mei 2023 Jijini Dar es Salaam. 

Tanzania ni moja kati ya nchi zilizopo Afrika Mashariki ambayo inakisiwa kuwa ni kitovu cha uzalishaji na uendelezaji wa madini mkakati na muhimu yanayotumika kutengeneza vifaa vitakavyosaidia matumizi ta nishati safi. Tanzania inavutia wawekezaji mbalimbali kutoka ulimwenguni kote kutokana na uwepo wa utajiri wa madini ya aina mbalimbali, sera rafiki na ongezeko kubwa na uhitaji wa nishati endelevu. 

Na pia Tanzania ni mwanachama wa Taasisi ya uhamasishaji, uwazi na uwajibikaji katika rasilimali madini, mafuta na gesi asilia(Extractive industries transparency Initiative-TEITI) inayozingatia uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa madini na maliasili kwa ujumla, Hatua hii inawapa wawekezaji uhakika kuwa sekta ya madini nchini inasimamiwa kwa umakini wa hali ya juu, uendelevu na yenye kuwajibisha. 

Serikali ya Tanzania kupitia wizara ya madini imezindua kongamano linalojulikana kama Tanzania mining and investment forum litakalofanyika kuanzia tarehe 25 mpaka 26 October 2023 na malengo ya mkutano huu ni pamoja na uwasilishaji taarifa muhimu za sekta ya madini, kuwa na vikao vya mazungumzo na wawekezaji, kubainisha fursa zilizopo kwenye miradi ya madini na kuimarisha ushirikiano wa ndani na nje ya nchi katika kukuza na kuifanya sekta ya madini kuwa endelevu. 

Kongamano hili la madini na uwekezaji litawavutia zaidi ya watu 2, 000 kutoka nchi zaidi ya 25 Ulimwenguni itakayoambatana na mkutano utakahodhi zaidi ya wazungumzaji 100,wenye zaidi ya vipindi 20,hotuba ya keynote na maonyesho makubwa ya teknolojia na uvumbuzi na kongamano la mwaka huu litaweka mazingatio makubwa zaidi kwenye uwekezaji wa Kimataifa, uchimbaji wa madink, miradi mipya, ushirikiano, teknolojia na uwezeshaji. 

Uzinduzi wa kongamano hili umezinduliwa leo na Waziri wa madini Dkt Dotto Biteko na kuwakaribisha wadau wa Madini katika kongamano hilo. 

"kwa heshima na taadhima ninayo furaha kubwa kuwakaribisha wageni wote waalikwa katika uzinduzi wa leo, Naomba kutumia fursa hii kuwakaribisha wadau wote waliopo kwenye sekta ya madini nchini Tanzania, bara la afrika na ulimwenguni kote, kushiriki kongamano la madini na uwekezaji litakalofanyika Dar es salaam tarehe 25 na 26 mwenzi October mwaka 2023"alisema Dkt Biteko

Kongamano la madini na uwekezaji imeandaliwa na Wizara ya madini pamoja na kampuni ya Dmg ambayo ni kampuni kubwa zinazoandaa halfa za kimataifa wakiwa na kumbukumbu ya halfa 84 katika tasnia mbalimbali wakiwavutia zaidi ya watu 425,000 kuhudhuria halfa hizo, Shughuli za Dmg zinahusiana na masuala ya nishati.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *