Mauzo ya Hisa (Turnover/ Liquidity)
Thamani ya mauzo ya hisa imepanda kutoka Shilingi Billioni 3 ya wiki iliyoishia 3 Novemba 2017 hadi Shilingi Bilioni 86 kwa wiki iliyoishia 10 Novemba 2017. Ongezeko hili kubwa la mara moja limetokana na ununuzi wa hisa za TBL kwa kampuni tanzu ya SABMiller
Vile vile Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imepanda kutoka hisa Mil 3.5 ya wiki iliyoishia 3 Novemba 2017 hadi hisa Mil 9 ya wiki iliyoishia 10 Novemba 2017.
Kampuni zilizoongoza katika mauzo ya hisa ni kama ifuatavyo:
TBL……………………………………………99%
CRDB………………………………………….0.56%
VODA………………………………………….0.01%
Ukubwa Mtaji (Market Capitalization)
Ukubwa wa mtaji wa kampuni zote zilizoorodheshwa katika soko umepanda kwa Shilingi Bilioni 525 kutoka Shilingi Trilioni 20.2 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 20.8 wiki iliyoishia tarehe 10 Novemba 2017. Ongezeko hilo limetokana na kupanda kwa bei za hisa za KCB (15%), NMG (10%), KA (9%) na TBL (1%).
Ukubwa wa mtaji wa kampuni za ndani umepanda kwa Shilingi Bilioni 29 kutoka Trilioni 10.051 hadi kafika Shilingi Trilioni 10.08 wiki hii. Hii ni kutokana na kupanda kwa bei ya hisa ya TBL (1%).
Kampuni
|
10 November 2017 (Shilingi)
|
3 November 2017 (Shilingi)
|
Badiliko (%)
| ||||
CRDB
|
0.00%
| ||||||
DCB
|
0.00%
| ||||||
DSE PLC
|
1,
|
0.00%
| |||||
MBP
|
0.00%
| ||||||
MCB
|
0.00%
| ||||||
MKCB
|
0.00%
| ||||||
MUCOBA
|
0.00%
| ||||||
NMB
|
2,750
|
0.00%
| |||||
PAL
|
0.00%
| ||||||
SWALA
|
0.00%
| ||||||
SWIS
|
3,500
|
0.00%
| |||||
TBL
|
13,300
|
0.76%
| |||||
TCC
|
16,800
|
0.00%
| |||||
TCCL
|
1,200
|
0.00%
| |||||
TOL
|
0.00%
| ||||||
TPCC
|
1,520
|
0.00%
| |||||
TTP
|
0.00%
| ||||||
VODA
|
0.00%
| ||||||
YETU
|
0.00%
| ||||||
Kampuni zilirodhodheshwa kutokea Masoko mengine
| |||||||
ACA
|
5,240
|
-3.50%
| |||||
EABL
|
5,410
|
2.27%
| |||||
JHL
|
10,420
|
7.64%
| |||||
KA
|
9.09%
| ||||||
KCB
|
14.63%
| ||||||
NMG
|
2,590
|
9.75%
| |||||
USL
|
0.00%
| ||||||
Mtaji Jumla Makampuni yote (Bilioni)
|
20,752
|
2.54%
| |||||
Mtaji Jumla Makampuni ya Ndani (Bilioni)
|
10,081
|
0.30%
| |||||
Kiashiria cha DSEI (pointi)
|
2,155
|
2.57%
| |||||
Kiashiria cha TSI (pointi)
|
3,845
|
0.29%
|
Viashiria (Indices)
Kiashiria cha kampuni zote zilizoorodheshwa katika soko yaani DSEI kimepanda kwa pointi 53 kutoka pointi 2,101 hadi 2,154 pointi hii ikiwa ni kutokana na kupanda kwa bei za hisa za Kenya Commercial Bank (KCB), National Media Group (NMG), Kenya Airways (KA), na Tanzania Breweries Ltd (TBL).
Pia kishiria cha kampuni za ndani yaani TSI kimepungua kwa pointi 11 kutoka pointi 3,833 hadi pointi 3,845 kutokana na kupanda kwa bei za hisa za TBL.
Kiashiria cha sekta ya viwanda (IA) kimepanda kwa pointi 26 kutoka pointi 5,303 hadi pointi 5,329
Kiashiria huduma za kibenki na kifedha (BI) wiki hii imebaki kama awali kwenye wastani wa pointi 2,464.
Kiashiria cha Sekta ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii imebaki kama awali kwenye wastani wa pointi 2,462
Hati Fungani (Bonds)
Mauzo ya hati fungani katika wiki iliyoishia tarehe 10 Novemba 2017 yalikuwa Shilingi Bilioni 11.2 kutoka Shilingi Bilioni 15.7 wiki iliyopita ya 3 Novemba 2017
Mauzo haya yalitokana na hatifungani saba (7) za serikali zenye jumla ya thamani ya Shilingi Bilioni 12.5 kwa jumla ya gharama ya Shilingi Bilioni 11.2
0 maoni:
Chapisha Maoni