WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumatano, 11 Novemba 2026

 20:27      No comments




 Na Jerome Mlaki wa Dar.

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Sauda Msemo, amesisitiza umuhimu wa kuharakisha matumizi ya mifumo ya malipo ya kidijitali katika biashara ili kuongeza ufanisi, kupunguza gharama na kukuza ujumuishwaji wa kifedha nchini na ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).


Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano kuhusu Uwezeshaji wa Malipo ya Kidijitali kwa Wafanyabiashara wa soko la Kkoo uliofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 11 Nov 2026, Bi. Msemo amesema kuwa licha ya mafanikio yaliyopatikana katika upanuzi wa huduma za kifedha za kidijitali, bado biashara nyingi za zinafanyika kwa kutumia fedha taslimu.


Amesema utegemezi huo wa fedha taslimu unasababisha changamoto mbalimbali za kimuundo, ikiwemo gharama kubwa za miamala, hatari za kiusalama, ukosefu wa uwazi pamoja na kuwanyima wafanyabiashara, hususan wanawake na vijana, fursa ya kupata huduma rasmi za kifedha.


Bi. Msemo alibainisha kuwa taarifa zilizokusanywa kutoka katika maeneo mbalimbali, zinaonesha wazi haja ya kuchukua hatua madhubuti na shirikishi ili kuondoa vikwazo vinavyokwamisha matumizi ya mifumo ya malipo ya kidijitali.


Alieleza kuwa mkutano huo ni fursa muhimu ya kujadili na kukubaliana juu ya vipaumbele na suluhisho zitakazochochea matumizi ya mifumo salama, nafuu na jumuishi ya malipo ya kidijitali katika biashara.


“Lengo letu la pamoja ni kujenga mfumo wa malipo unaoweza kuunganika, unaopatikana kwa urahisi, wenye gharama nafuu na unaoaminika, ili kuwezesha miamala ya kibiashara kufanyika kwa urahisi na kuchochea ushirikiano wa kiuchumi” alisema.


Aidha, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa karibu kati ya taasisi za umma, wadau wa sekta ya fedha, watoa huduma za kifedha na wabunifu wa teknolojia katika kufanikisha azma hiyo, huku akibainisha kuwa ni muhimu pia kuhakikisha suluhisho zinazopatikana zinazingatia mahitaji halisi ya wafanyabiashara.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *